Fatuma Mshamu na Josephine Burton
MKAZ I wa Ki b a
h a Kongowe aliyetambulika kwa jina la Albert Madeje (30) amefariki dunia baada
ya kugongwa na gari wakati akivuka barabara.
Tukio hilo lilitokea Juni 30, mwaka huu
majira ya saa tatu kamili usiku alipokuwa akivuka barabara ya Morogoro eneo la
Mbezi Mwisho.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo,
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camillius Wambura alisema ajali
hiyo ilihusisha gari namba aina ya BWM iliyokuwa ikiendeshwa na Herman
Berege.
Kamanda huyo alisema, dereva huyo alikuwa
akitokea Mbezi kwa Yusuph akielekea Kimara.
Alisema, alipofika maeneo hayo alimgonga
mwenda kwa miguu huyo aliyekuwa akivuka barabara.
Katika ajali hiyo, Wambura alisema, Albert
alifariki papo hapo.
"Baada ya kutokea ajali hiyo madereva
wa bodaboda wa eneo hilo walijichukulia sheria mkononi na kumshambulia dereva
huyo.
"Kwa kumpiga mawe, fimbo na kumjeruhi
sehemu mbalimbali za mwili na kuharibu gari lake kwa kulivunja vioo kwa mawe na
kumpora mali alizokuwa nazo kwenye gari," alisema.
Hata
hivyo, Kamanda huyo alisema maiti imehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala
na dereva amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo hakuna aliyekamatwa na
upelelezi unaendelea
No comments:
Post a Comment