Na Queen Lema, Arusha
MWENYEKITI kamati ya usafi Mkoa wa Arusha, Adolf Ulomi amesema kuwa
kampeni ya usafi wa Jiji la Arusha bado inakabiliwa na changamoto kubwa hasa ya
baadhi ya wanasiasa kuingiza siasa kwenye suala hilo jambo ambalo wakati
mwingine linafanya jiji kuonekana bado chafu.
Ulomi
aliyasema hayo jana katika eneo la Kwa Muorombo wakati Kamati hiyo ikiendelea
na usafi wa Jiji na kuhusisha wananchi pamoja na wafanyabiashara wa eneo hilo. Alisema
kuwa pamoja na kuwa kamati hiyo ya usafi imejizatiti katika kuhakikisha kuwa
Jiji la Arusha linakuwa safi lakini baadhi ya wanasiasa wa Mkoa wa Arusha
wanatumia vyeo vyao kupotosha maana halisi ya Kamati hiyo lakini pia umuhimu wa
jiji kuwa safi.
Alifafanua
kuwa baadhi ya wanasiasa hao mara nyingine wanadai kuwa wanawaonea huruma
wananchi hasa wale ambao wanaharibu mazingira huku baadhi ya wananchi hao nao
wakitumia muda huo kuchafua mazingira kwa kisingizio kuwa wamepewa ruhusa na
wanasiasa wao.
P i a a
l i s ema wa n a s i s a s a wanatakiwa kuiga mfano wa usafi kwenye miji
mingine ambayo imeendelea duniani na hata baadhi ya miji hapa nchini ukiwemo
mji wa Moshi jinsi ambavyo wameungana na kisha kuwabana baadhi ya wananchi
wanaochafua mazingira jambo ambalo limekubalika na limejengeka kuwa usafi ni wa
jamii na wala sio wa Serikali.
Wakati
huohuo aliishauri Serikali kuwa inatakiwa kuwa bunifu zaidi kwenye sekta ya
uwekezaji kwani kama sekta hiyo ikiwa ni kubwa hata wafanyabiashara
wadogowadogo ambao wakati mwingine wanauza bidhaa zao bila kujali usafi wa mji
wataweza kuwa na ajira.
Ulomi alifafanua kuwa kwa sasa katika mji wa Arusha asilimia kubwa ya
wafanyabiashara wadogo wamesambaa kila kona lakini kama kungekuwa na fursa za
uwekezaji basi wangezitumia vyema hivyo hata usafi ungeimarika zaidi.
No comments:
Post a Comment