26 July 2013

WAHOJI MATUMIZI YA SARAFU MOJA MUUNGANO



Na Mwajuma Juma, Zanzibar
WAJUMBE wa Baraza la Katiba wa Wilaya ya Mjini wamesema kuwa kuendelea kuwepo kwa sarafu moja na Benki Kuu moja katika mambo ya Muungano ni kuumiza sehemu moja kiuchumi. Wakizungumza katika mkutano wa baraza hilo uliofanyika mjini Unguja wajumbe hao walisema kuwa uchumi wa nchi hizo mbili ni tofauti kutokana na Zanzibar uchumi wake ni huduma na Tanganyika ni wa rasilimali ambao hauwezi kulinganishwa na uchumi wa Zanzibar.

"Zanzibar uchumi wake ni huduma, Tanganyika ni wa rasilimali hivyo kuendelea kuwa na Benki Kuu moja ni kuumiza sehemu moja ya Muungano hasa Zanzibar ambayo uchumi wake ni wa huduma," alisema mjumbe kutoka Shehiya ya Malindi Mustafa Bakari Sharif.
Alisema kuwa imefika wakati sasa kila nchi iweze kusimamia masuala yake yenyewe ya nchi ili kuweza kuendesha nchi yake kitaifa na kimataifa. Kuhusu masuala ya nje alisema kuwa kuwepo kwake katika orodha ya Muungano ni kuzikosesha nafasi nchi mbili hizo kutambulika kimataifa, hivyo ni vyema wakaachiwa kila nchi iendeshe nchi yake kimataifa.
Nae Firdausi Abdulrahman alisema kuwa rasimu iliyopo ya kutengeneza katiba mpya haioneshi kutambua ushirikiano pamoja na nembo ya Taifa kutoonesha sura ya ushirikiano wao.
Sambamba na hilo alisema kuwa ipo haja ya kuanzishwa utaratibu maalumu wa uingiaji wa watu ili kuepusha kujitokeza ongezeko la watu hasa

1 comment:

  1. Mambo yote saba yaliyopendekezwa na tume yawe ya muungano bado si suluhisho la kuifanya nchi kuwa na mamlaka kamili.
    Hoja za msingi zilizotolewa hapa zinapaswa ziangaliwe upya na tume ya mabadiliko ya katiba.
    inapaswa kwanza kuundwa katiba ya Tanganyika na ile ya watu wa Zanzibar kisha yawepo majadiliano ya kipi kiingizwe kwenye muungano ambacho hataumiza upande wowote.

    ReplyDelete