30 July 2013

WANAOVAA VIBAYA WADHIBITIWENa Martha Fataely, Mwanga
WAKAZI wa Kijiji cha Uchira wameomba s u a l a l a ma v a z i kuwekwa kisheria ili kukabiliana na ukiukwaji wa maadili unaofanywa sasa na baadhi ya wanawake na wanaume na kuchangia kuwapo kwa maambukizi mapya ya Ukimwi.

Kutokana na hilo, wameomba ziwekwe sheria ndogo ndogo ambazo zitakuwa zikitoa adhabu zikiwamo faini kwa wale wote watakaozikiuka na hivyo kupotosha maadili kwa kizazi kijacho.
Wakizungumza wakati wa mdahalo wa usawa wa kijinsia ulioandaliwa na Shirika la Mazingira mkoani Kilimanjaro (KENOT) kwa ufadhili wa The Foundation for Civil Society, Theresia Msuya na Ajenta Lyimo wamesema itasaidia kulinda utu.
"Jinsi mavazi yanavyovaliwa sasa, ipo haja kwa halmashauri za wilaya na manispaa kwa kushirikiana na serikali, kuunda sheria hizo ambazo zitalinda maadili, lakini pia kupunguza matamanio ya kushiriki ngono yanayochangiwa na mavazi," alisema.
Katika hatua nyingine baadhi ya wauguzi kwa kushirikiana na ndugu wa wagonjwa wamedaiwa kuwafanyia ukeketaji wanawake wa j awa z i t o wa k a t i wa kujifungua na hivyo kuwaathiri kisaikolojia.
Akizungumza wakati wa mdahalo huo, Mjumbe wa KENOT, Josephine Mfaume a l i s ema v i t e n d o h i v y o vimeshamiri zaidi katika wilaya ya Rombo huku wanawake husika wakibaini kufanyiwa hivyo hutakiwa kutunza siri vingine hutengwa na ukoo.
Aidha alisema kuwa ushuhuda wa kufanyika kwa vitendo hivyo pia ulitajwa katika siku 16 za kupinga ukatili ambapo baadhi ya wanawake wa wilaya hiyo walielezea na kuomba ushauri na msaada wa kisheria ili kukomesha vitendo hivyo.
Hata hivyo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Faisal Issa alikanusha kuwapo kwa madai hayo lakini akaahidi kufuatilia ili kama kuna ukweli wahusika wasakwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Pamoja na kauli hiyo lakini katibu wa hospitali ya mkoa huo, Boniface Lyimo alikiri kusikia malalamiko hayo ambayo hata hivyo alidai hayakuwa na uthibitisho ingawa juhudi za kufanyia uchunguzi zimeanza  

No comments:

Post a Comment