Chamacha Wakulima
Tanganyika (TFA) kimesema kuwa wananchi wa Kanda ya Kaskazini wanatakiwa
kujiwekea akiba ya vyakula kwani mikoa hiyo huenda ikakabiliwa na ukame mkubwa
kutokana na baadhi ya wakulima kukosa pembejeo za msingi huku wengine mpaka
sasa mazao yao
yakiwa yamedumaa mashambani, anaripoti Queen Lema, Arusha.
Hata hivyo, kwa kipindi hiki Kanda hiyo
ya Kaskazini itakabiliwa na kiwango cha zaidi ya asilimia 40 cha ukame tofauti
na msimu wa mavuno wa mwaka jana ambacho kilikuwa chini ya asilimia hizo.
Ha y o y a l i e l e zwa n a Mwenyekiti
wa chama hicho, Elias Mshiu wakati akizungumza kwenye mkutano wa 56 wa chama
hicho uliofanyika katika eneo la TFA Shoprite Jijini Arusha mapema jana.
Ms h i u a l i s ema k uwa tahadhari
hiyo inapaswa hata kuchukuliwa na jamii yote ya Kanda ya Kaskazini kwani mpaka
sasa baadhi ya maeneo hayana mazao kabisa hali ambayo wakati mwingine
inaashiria baa la njaa kwa msimu ujao wa chakula.
Akielezea chanzo kikubwa cha wakulima
wengi kukosa mazao kwa msimu ujao wa mavuno alisema kuwa sababu kubwa kabisa ni
ukosefu wa pembejeo za kilimo kwa wakati kwani toka msimu wa kulima na kupanda
bado zilikuwa hazijafika na hatimaye baada ya zoezi la upandaji ndipo pembejeo
hizo zilipofika,
Aliongeza kuwa hali hiyo ilisababisha
baadhi ya wakulima kulima, kupanda bila pembejo ikiwemo mbolea jambo ambalo
limesababisha baadhi ya mashamba kukosa mazao lakini pia hata yale ambayo
yametoka nayo hatyaridhishi kwa matumizi ya chakula na biashara.
"Tahadhari kubwa inatakiwa
kuchukuliwa kwani msimu ujao wa mavuno haki itakuwa ni tete sana na sasa huenda
mikao hii ya kaskazini ikakumbwa na njaa kali kuliko ile ya mwaka jana lakini
pia kama tahadhari itachukuliwa mapema itasaidia hata kuweka akiba hususani
kwenye familia zile ambazo hazina uwezo," aliongeza Mshiu.
Awali, alisema kuwa kwa sasa hata
kilimo cha Kanda ya Kaskazini bado kinakabiliwa na changamoto kubwa sana kwani
baadhi ya wakulima wanategemea zaidi majira ya mwaka huku hali hiyo
ikisababisha wengi kukosa mazao
Mshiu aliongeza kuwa kama uwekezaji
mkubwa utawekwa kwenye kilimo cha umwagiliaji basi kanda ya kaskazini itakuwa
ni miongoni mwa kanda zenye vyakula vya kutosha kwa ajili ya matumizi ya
vyakula, lakini pia kwa ajili ya biashara.
Katika hatua nyingine,
wakulima wa chama hicho waliiomba Serikali na wadau wengine wa kilimo kuweka
mikakati mbalimbali ambayo itaweza kuboresha zaidi kilimo cha umwagiliaji kwani
aina ya kilimo ambacho kinafanyika kwa sasa cha kutegemea zaidi majira ya mwaka
ni cha kubahatisha kwani kilimo cha umwagiliaji ni cha majira yote ya mwaka.
No comments:
Post a Comment