Na Mashaka Mhando, Tanga
WAZAZ I wa wa t o t o
wanaosoma katika Shule ya Msingi Azimio iliyopo Kata ya Makorola katika Jiji la
Tanga, wameonesha wasiwasi wao wa kutokea magonjwa ya mlipuko kutokana na shule
hiyo kukosa vyoo kwa matuminzi ya wanafunzi.
Mmoja wa wazazi waliokuwa na watoto wanaosoma katika shule hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Papaa Bokande, alisema shule hiyo imekuwa haina maji, vyoo na mlinzi licha ya wazazi kutoa michango kila mwezi kuchangia gharama hizo.
"Kwa kweli tunasikitika watoto wetu wanasoma katika shule
ambayo haina vyoo, maji na mlinzi, tuna wasiwasi kunaweza kutokea magonjwa ya
mlipuko pale ni hatari sana na sisi tumekuwa tukichanga fedha kila mwezi,"
alisema Bokande.
Alisema mwezi uliopita walifanya kikao na mwalimu mkuu wa shule
hiyo aliyemtaja kwa jina moja la Mndolwa ambapo walikubaliana kuishinikiza
halmashuari ya jiji kujenga vyoo kwa ajili ya kuokoa watoto wao lakini wanaona
kama suala hilo halishughulikiwi.
Mwandishi wa habari hizi alipofika shuleni hapo mwishoni mwa wiki,
hakuweza kumkuta Mkuu huyo wa shule ambapo mmoja wa walimu aliyekutwa hapo
alisema mkuu wao amekwenda halmashauri ya Jiji kwenye vikao vyao vya mwishoni
mwa wiki.
Hata hivyo, mwalimu huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe
gazetini, alisema kuwa shule hiyo iliyoanzishwa miaka sita iliyopita, inatumia
vyoo vya shule mama iliyopo jirani na shule hiyo ya Makorola ambayo wanafunzi
wote wanatumia vyoo hivyo.
"Mwalimu Mkuu hayupo amekwenda ofisi za Jiji, lakini
suala hilo la shule kukosa vyoo si kweli wanafunzi wanatumia vyoo vya shule
mama ya Makorola lakini mpango wa kuchimba vyoo upo ni utekelezaji tu wa suala
hili," alisema mwalimu huyo.
No comments:
Post a Comment