Na Florah Temba, Moshi
WAKUL IMA 1 , 0 0 0 wa
kahawa katika wilaya sita za Mkoa wa Kilimanjaro na Arumeru mkoani Arusha,
wanatarajia kunufaika na mradi wa kuwajengea uwezo juu ya usajili na uhakiki wa
kahawa yenye ubora lengo likiwa ni kuwawezesha kutekeleza mbinu bora za kilimo
endelevu na kujikwamua kiuchumi. Mradi huo wa kuwajengea uwezo wakulima wa kahawa juu ya usajili na
uhakiki wa kahawa yenye ubora katika nchi wanachama wa Shirika la Kahawa
Mashariki mwa Afrika (EAFCA) ulianza kutekelezwa kwa ufanisi nchini Tanzania
Julai 2011 ambapo utamalizika mwaka 2015 na unatarajiwa kuwafikia wakulima
zaidi ya 1,000.
Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa kutolewa mafunzo kwa
wanachama zaidi ya 40 wa chama cha msingi cha Kibong'oto Wanri, mtafiti wa
usambazaji teknolojia na mafunzo katika taasisi ya utafiti wa kahawa Tanzania
(TaCRI), Jeremiah Magesa alisema taasisi hiyo inawajengea wakulima uwezo na
kuwatafutia soko la uhakika la kahawa.
Alisema lengo hasa la mradi huo ni kuwawezesha wakulima kuzalisha
kahawa yenye ubora ambayo itakubalika katika soko hali ambayo itawawezesha
kuongeza kipato na kuondokana na lindi la umaskini. "Wakulima 1,000 katika wilaya za Rombo, Hai, Siha, Mwanga,
Moshi vijijini, Same mkoani Kilimanjaro na wilaya ya Arumeru mkoani Arusha
watafundishwa juu ya usajili na uhakiki ili kukidhi vigezo vinavyohitajika
katika soko, kutokana na ukweli kwamba soko la kahawa kwa sasa linaangalia
ubora," alisema Magesa.
Kwa upande wao baadhi ya wakulima wa kahawa Kibong'oto Wanri
waliipongeza taasisi ya TaCRI kwa kuwapatia mafunzo hayo na kusema kuwa
yamewawezesha kujitambua na kuzingatia kanuni bora za kilimo cha kahawa hali
ambayo wanaamini itawawezesha kuingia kwenye ushindani wa soko la kahawa la
kitaifa na la kimataifa. Amini Munuo alisema wakulima wengi wamejisahau na kuendeleza
kilimo cha zamani kisicho na tija hali ambayo imewafanya kukosa soko la uhakika
na kuathirika kimapato.
Alisema mafunzo hayo waliyopewa ni msaada mkubwa kwao katika
kuhakikisha wanaboresha kilimo cha kahawa na kuzalisha kahawa bora ambayo
itakubalika katika masoko ya kimataifa na hatimaye kuongeza kipato na kupiga
vita adui umaskini.
Naye Meneja wa Mradi huo Afrika, Filtone Sandando alisema
wanahitaji vizazi vijavyo vinufaike na mradi huo na kuhakikisha wanazalisha
kahawa bora ambayo itawawezesha kuongeza kipato chao. A l
i s e m a w a m e l e n g a kuwasaidia wakulima kupata bei nzuri ya kahawa
pindi watakapozingatia kanuni za kilimo bora cha kahawa hatua ambayo
itawawezesha kujikwamua kiuchumi
No comments:
Post a Comment