29 July 2013

WAKAZI TEMEKE KUJISAJILI NIDA



 Na Grace Ndossa
 MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imewataka wakazi wa Wilaya ya Temeke kujitokeza kwa wingi kwenye mchakato wa kuchukua alama za vidole, picha na saini zao .Kwa mu j i b u wa t a a r i f a iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu, Dicksoni Maimu, ilieleza kuwa watu watakaoanza kuchukuliwa alama hizo ni wa Tarafa ya Mbagala kata ya Kijichi, Tuangoma, Mbagala Kuu, Charambe, Kiburugwa mtaa wa Juhudi na Kiburugwa namba tatu
.Pia alieleza kuwa wahusika wote waliojaza fomu za maombi ya vitambulisho vya Taifa majina ya waombaji yamebandikwa kwenye mbao za matangazo katika vituo vya usaili.Hata hivyo, taarifa hiyo iliwataka wafike na nyaraka halisi za kuthibitisha uraia na umri pamoja na cheti cha kuzaliwa, pasipoti, vyeti vya elimu ya msingi na sekondari leseni ya udereva kitambulisho cha kupiga kura au pasipoti.
"Kwa ajili ya ubora wa picha unashauriwa kutovaa nguo nyeupe, kijivu, bluu mpauko pinki au kofia ili picha iweze kutoka vizuri,"alisemaPia aliwataka wakazi wa maeneo mengine wavute subira kwani shughuli ya uchukuaji alama za vidole picha na saini linakwenda kwa awamu na shughuli hiyo ni bure

No comments:

Post a Comment