Na
Mwandishi Wetu, Tanga
KOCHA
Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelu 'Julio' amesema timu hiyo inahitaji mechi
tatu za kirafiki kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara,
inayaotarajia kuanza Agosti 24, mwaka huu.Timu hiyo jana ilitarajia
kucheza mechi ya kirafiki na Coastal Union ya
jijini hapa, ambayo ilichezwa Uwanja wa Mkwakwani.
Akizungumza jijini hapa jana baada ya mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika asubuhi, kocha huyo alisema mechi ya kwanza watacheza na siku ya Simba 'Simba Day' na nyingine mbili watatoka nje ya Dar es Salaam.Kocha huyo alisema lengo lao ni kuhakikisha wanajiandaa vyema kwa ajili ya kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu, ambao wamenyang'anywa na watani wao wa jadi Yanga.
"Msimu huu tumepania kuanza ligi kwa kishindo
na kuhakikisha tunatwaa ubingwa na kushiriki michuano ya kimataifa,"
alisema Kocha huyo.Simba ipo
jijini hapa tangu juzi na jana asubuhi ilifanya mazoezi Uwanja wa mkwakwani kwa
ajili ya kujiandaa na mechi dhidi ya Coastal Union..
No comments:
Post a Comment