Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Vital'O ya Burundi juzi usiku
ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Afrika Mashariki na Kati maarufu kama
Kagame baada ya kuifunga APR ya Rwanda mabao 2-0.
Mechi hiyo iliyokuwa na upinzani mkali
ilichezwa Uwanja wa El Fasher Jimbo la Darfur Kaskazini nchini Sudan.
Waliokuwa mashujaa wa Vital'O ni Amisi
Tambwe aliyefunga bao dakika ya 63 na Deo Ndayishimiye ambaye alifunga dakika
ya 65.
Vital'O chini ya kocha wake mpya
Mnyarwanda Yaounde Kanyankore ilifanikiwa kutawala mchezo na kuidhibiti ipasavyo
APR ambao walitaka kuchukua kombe hilo lililopachikwa jina la Rais wao Paul
Kagame, lakini ngome ya Warundi hao ilikuwa imara.
Mwaka jana Yanga ndio waliokuwa mabingwa
wa kombe hilo, lakini mwaka huu timu za Tanzania hazikushir
iki michuano hiyo kwa kuhofia hali ya
usalama nchini Sudan.
Katika michuano hiyo bingwa ambao ni
Vital'O waliondoka na kitita cha dola za Marekani 30,000, washindi wa pili APR
ya Rwanda dola 20,000 na mshindi wa pili ni wenyeji El Merreikh walishika
nafasi ya tatu na kupata dola 10,000, wenyeji hao
Na Mosi Mrisho
MBIO za kuwania madaraka ndani ya
Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), zimeanza na zinatarajiwa
kuhitimishwa jijini Mwanza kesho ambapo uchaguzi huo utafanyika.
Akizunmgumza Dar es Salaam jana Afisa
Michezo Msaidizi wa BFT Richard Mganga, alisema mpaka sasa wamejitokeza watu
watano kuchukua fomu za kuwania uongozi ndani ya chama hicho.
Maganga alisema uchaguzi huo utafanyika
baada ya viongozi wa sasa kumaliza muda wao wa uongozi kwa mujibu wa katiba ya
chama hicho.
Alisema wapo watu wengi wanaohitaji
kuingia kwenye uongozi huo, lakini zipo sifa mbalimbali ambazo zinahitajika ili
kuweza kushiriki uchaguzi huo.
Maganga aliongeza kuwa wadau kabla ya
kufikiria kuingia BFT lazima wagombea wajichuje wenyewe, ambapo mgombea pamoja
na elimu yake au kuwa na sifa nyengine anatakiwa kuwa na sifa za uongozi
nauzoefu wakutosha.
Alisema
mpaka sasa waliojitokeza kuchukua fomu za kuomba uongozi ni watano.
No comments:
Post a Comment