Na Mwandishi Wetu
TIMU y a Ki n o n d o n i wasichana imeanza vizuri michuano ya vijana
chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars 2013 ngazi ya Taifa, kwa
kuwafunga mahasimu wao timu ya Ilala 2-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa
kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam jana.
Kinondoni waliuanza
mchezo huo kwa kasi mara tu baada ya kipenga cha kwanza kupulizwa na juhudi zao
zilizaa matunda dakika ya tano wakati mchezaji Anna Ebron alipoachia shuti la
mbali na kwenda moja kwa moja wavuni na kumuacha mlinda mlango wa timu ya Ilala
akichupa bila mafanikio.
Goli hilo
liliamsha hamasa kutoka kwa mashabiki wa Kinondoni.
Baada ya hapo
Ilala walianzisha mashambulizi na kulisakama lango la wapinzani wao kwa lengo
la kupata goli la kusawazisha lakini walinzi wa timu ya Kinondoni wa l i k uwa
ma k i n i k u o k o a mashambulizi hayo.
Kwa u j uml a
Ki n o n d o n i walionesha mchezo mzuri na pengine wanaweza kutimiza ndoto yao
ya kutwaa kombe ya ARS upande wa wasichana mwaka huu.
Timu zote
zilianza kipindi cha pili kwa ari mpya na kupata nafasi kadhaa za kufunga na
ilikuwa ni Kinondoni tena waliofanikiwa kupata goli katika dakika ya 56 kupitia
kwa Rehema Yahya baada ya kupata krosi kutoka upande wa kulia na kufunga goli
la pili.
Mechi hiyo
ilifuatiwa na mchezo mwingine kati ya Kinondoni na Temeke wavulana ambapo
Kinondoni ilishinda 2-1. Mchezo huo ulikuwa mkali na ulivuta hisia za wapenzi
na wadau wengi wa soka akiwemo kocha wa timu ya taifa ya vijana Jacob Michelsen
ambaye alisifu kiwango cha mchezo kilichooneshwa na timu hizo.
"Nafikiri michezo hii itatoa fursa
nzuri ya kubaini vipaji vya wachezaji chipukizi na kusema kweli itatusaidia
kupata timu ya vijana ya Taifa chini ya umri wa miaka 17 ambayo tutaiunda hivi
karibuni," alisema Michelsen baada ya kushuhudia mechi hizo za mwanzo.
Katika mchezo wa wavulana Kinondoni
walikuwa wa kwanza kutikisa goli la wapinzani wao wakati mchezaji machachali
Mustafa Yusuf alipopata krosi kutoka upande wa kulia na kuunganisha mpira
wavuni kwa shuti kali.
Goli hili lilibadili kasi ya mchezo huku
Temeke wakishambulia kwa nguvu na kufanikiwa kupata goli la kusawazisha dakika
ya 28 kupitia kwa Salum Issa.
Kipindi cha pili Kinondoni waliutawala
mchezo kwa kosa kosa nyingi na alikuwa Willy Kalolo aliyewainua washabiki wa
timu hiyo baada ya walinzi wa Temeke kufanya uzembe na kumuwezesha mfungaji
kupata mpira kwa urahisi katika eneo la hatari na kufunga goli la kuongoza
katika dakika ya 50.
Mashindano ya Airtel Rising Stars mwaka
huu yanashirikisha timu kutoka mikoa ya kisoka ya Ilala, Kinondoni, Temeke
(wasichana na wavulana), Mwanza, Morogoro, Mbeya (wavulana), Tanga, Ruvuma na
Kigoma (wasichana).
Timu
ziliwasili jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kufanyiwa uhakiki wa umri
tayari kwa mashindano ya ngazi ya Taifa ambayo yalitarajiwa kufunguliwa rasmi
na Naibu Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Kassim Majaliwa.
No comments:
Post a Comment