15 July 2013

VIONGOZI MTANADAO DAWA ZA KULEVYA WANYONGWE - CUF


Na Ignas Andrew
MW E N Y E K I T I wa Ch ama c h a Wananchi(CUF) W i l a y a y a Kinondoni, Juma Nkumbi amesema serikali inatakiwa kuwanyonga viongozi wanaohusika na mtandao wa dawa za kulevya ili iwe fundisho.
Hayo aliyasema jana, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na mwenendo mzima wa mmong'onyoko wa maadili wa vijana ambao ndio nguvukazi ya Taifa lijalo.

Akizungumza na jana, mwenyekiti huyo ambaye pia ni diwani wa kata ya Kibada wilaya ya Temeke, alisema kuwa, Taifa linaendelea kumong'onyoka kimaadili kwa kuwa uwajibikaji wa serikali ni kimazoea; hivyo ameitaka kuhakikisha anatumia sera ya nchi ya China kwa kuanza kunyonga viongozi wote wanaohusika.
"Uwajibikaji huu wa kimazoea ndio unaomaliza Taifa,wakati vitu vipo wazi sidhani kama kweli serikali haifahamu wanaoyaingiza madawa hayo,lakini hakuna hatua zinazochukuliwa kwa kuwa pamekuwapo na rushwa; na urafiki," alisema Nkumbi.
Wa k a t i h u o h u o ; mwenyekiti huyo ameyataka mabaraza ya kaya ya katiba kuhakikisha wanaipitia ipasavyo rasimu mpya ya Katiba ili kutoa maoni ambayo yanatachangia kupata kanuni na sheri bora.
"Wajumbe wa mabaraza ya katiba hakikisheni mnaipitia vizuri katiba kwanza,kabla ya kuitolea maamuzi,na maoni ili tupate miongozo sahihi ambayo itatumika kama kanuni za utawala bora,badala ya kuwa na bora utawala," alisema Nkumbi.
Alisema kuwa inasikitisha mno kuona jamii inaendelea kupoteza nguvukazi ya Taifa ambayo inaangamia kwa matumizi ya dawa za kulevya kwa sababu ya manufaa ya watu wachache ambao wametazama na kujali maisha yao na kulitupa Taifa.
Aidha, kwa upande mwingine Mwenyekiti huyo amelaani vikali vitendo vinavyofanywa na mamlaka ya Dawa na Chakula nchini (TFDA) kwa kuidhinisha matumizi ya dawa zisizofaa kwa jamii.
"Lingine ambalo nalipigia kelele hivi ni kweli Mamlaka ya Dawa na Chakula inawezaje kupitisha dawa zisizofaa,hali ambayo inapelekea jamii ya Watanzania kupoteza uhai halafu bado Serikali inatazama tu?" alihoji mwenyekiti huyo.

No comments:

Post a Comment