MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wilayani Handeni, imemwachia huru Mkazi mmoja wa
Kijiji cha Kwamnele kilichopo Kata ya Ndolwa, Mohamed Rajab (38) ambaye alikuwa
akikabiliwa na shtaka la kukutwa na viungo vya binadamu kinyume cha sheria.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo, Patrick
Maligana, alisema kuwa ushahidi uliotolewa mahakamani hapo haukuwa wa moja kwa
moja wa kuweza kumtia hatiani mshtakiwa.
Alisema mashahidi wa tukio hilo walitoa ushahidi ambao hauwezi k u t h i
b i t i s h a k u w a mtuhumiwa anahusika na tukio hilo kwa kueleza mambo
tofauti, hivyo mahakama inamwachia huru mtuhumiwa na rufaa kwa washtaki ipo
wazi.
Awali,
Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Nzagalila Kikwelele alidai mahakamani hapo kwamba
mnamo Machi 2 mwaka 2011 mtuhumiwa huyo alikamatwa kwa kosa la kukutwa na
viungo vya binadamu nyumbani kwake.
A l i s e m a
katika upekuzi u l i o f a n y w a chumbani kwake alikutwa na fuvu la binadamu,
taya na mifupa ya mbavu vikiwa vimefukiwa nyuma ya nyumba yake huku pembeni ya
eneo hilo kukiwa na sanda.
Hata hivyo,
alipotakiwa kujitetea kabla ya hakimu huyo kutoa hukumu, mshtakiwa huyo
aliieleza mahakama hiyo kwamba hahusiki na vitu hivyo na kuitaka mahakama
imwachie huru kwa kuwa kosa lililoletwa mbele ya mahakama hahusiki nalo huku
akilitaka Jeshi la Polisi kumtafuta tena mmiliki halali wa viungo hivyo.
Mshtakiwa huyo,
aliendelea kudai mahakamani hapo kwamba, siku ya tukio hilo hakuwepo nyumbani
kwake
alikuwa
shambani akilima kama ilivyo kawaida yake, lakini alishangaa aliporudi nyumbani
akiwa na jembe lake begani, akawakuta polisi wamejaa nyumbani kwake na
wakamkamata.
No comments:
Post a Comment