29 July 2013

VIJANA WATEMA CHECHE URAIS 2015



 Na Goodluck Hongo
KAMATI ya Vijana Wapenda Ama n i Ta n z a n i a (KVT ) ime w a t a k a Wa t a n z a n i a kujihadhari na watu wanaotaka urais kupitia vyombo vya habari, makanisani na misikitini kwani watakapoingia madarakani ni rahisi kuvuruga amani ya nchi kwa kutekeleza yale ya upande mmoja na kuacha mwingine.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa KVT, Chifu Msopa, alisema hali ya kisiasa kwa sasa si nzuri na kuna hatari kuwapitisha viongozi wanaopita makanisani na misikitini, wale wenye nia ya kulipa visasi.

Kamati hiyo inajumuisha vijana kutoka katika vyama vyote na dini kutoka mikoa yote nchini.Alisema wao wakiwa kama viongozi wana wajibu wa kusema pale ambapo hali inaenda vibaya kutoka kwa wale wanaojitosa kwenye mbio za kuwania urais.Alisema taasisi hiyo imejadili kwa kina vijana kupendekezo wanaofaa kuwania nafasi hiyo na kutokana na kuwa na sifa nzuri.
"Kwa upande wa vijana tumeona watu wenyewe sifa za kugombea urais ni wanne tu," alisema.Aliwataja vijana wanaofaa kuwania urais kuwa ni Zitto Kabwe, James Mbatia,January Makamba na Dkt.Hussein Mwinyi. Alisema sifa kubwa z a wa t u h a o n i we n y e maadili,hawana chuki wala visasi ndani ya vyama vyao na nje ya vyma vyao.
"Lakini pia si viongozi wababe wala hawana chembechembe za udikteta na uongozi wa kiimla, ni viongozi ambao wanawaunganisha Watanzania kwa dini zao makabila yao kanda zao pande zao,"alisema.
Alibainisha kuwa wao kama kamati ya vijana wamegundua kuwa watu wamekuwa na visasi na kuonya kuwa kama atachaguliwa mtu ambaye anapita makanisani na misikitini na baada ya kupata urais akashindwa kulipa fadhila kwa Wakristu au Waislamu atasababisha migogoro.Aliongeza kuwa, kama vyama vyao vitateua majina ya wanasiasa hao vijana taasisi hiyo itakuwa wapo tayari kuzunguka nchi nzima kuwapigia debe ili washinde urais.
Naye Katibu Mkuu wa Kamati hiyo, Sadiki Godigodi, alisema taasisi hiyo ina vijana kutoka pande zote za nchi na kazi yake ni kuhimiza amani, upendo, umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania. Alisema kazi yake nyingine ni kuhimiza vijana kujitolea.
Alisema japo kwa sasa si njia sahihi ya kujadili majina ya wagombea urais, lakini nyufa alizowahi kusema Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julias Nyerere zimeanza kuonekana, ikiwemo chuki kati ya viongozi wa kisiasa walio ndani ya chama kimoja, kuongezeka uadui wa kisiasa baina ya vyama vya siasa,kushuka vya ufanisi na weledi katika taasisi muhimu kama bunge, mahakama na polisi.
"Katika nchi inayohitaji mabadiliko kama nchi yetu uzoefu wa miaka mingi wa siasa si kipimo kizuri cha uongozi bora kwani kwa sasa nchi hii haihitaji uzoefu wa siasa ila kinachotakiwa ni kwamba ili chama kishinde kinapaswa kuteua mgombea anayeshabihiana na Watanzania walio wengi ambao ni vijana," alisema Godigodi

No comments:

Post a Comment