26 July 2013

VIJANA WA KISHAPU KOKOPESHWA PIKIPIKI



 Na Suleiman Abeid, Kishapu

 MB U N G E w a J i m b o la Kishapu mkoa wa Shinyanga, Suleiman Nc h amb i ame z i n d u a rasmi mpango wa kuvikopesha pikikipiki kwa masharti nafuu ya bila riba yoyote vikundi vya vijana wanaoendesha pikipiki za bodaboda wilayani humo.Akizungumza kwenye sherehe fupi ya mapokezi ya pikipiki 20 za awali zilizogharimu kiasi cha sh.milioni 42 zilizofanyika juzi katika kata za Bubiki, SekeBugolo, Mwigumbi na Songwa, Nchambi alisema mpango huo ni moja ya ahadi zake alizozitoa wakati wa kipindi cha kampeni mwaka 2010
. Kila kijana atakayekopeshwa pikipiki kupitia kikundi chake atapaswa kulipia asilimia 30 ya bei halisi ya pikipiki ambapo kiasi kinachosalia kitalipwa kwa utaratibu utakaopangwa na vijana wenyewe na baada ya kukamilisha marejesho pikipiki itamilikiwa na kijana aliyekopeshwa.Nchambi alisema mbali ya kutekeleza ahadi hiyo lakini pia anaamini kupitia pikipiki hizo vijana wengi wilayani Kishapu wataweza kujiajiri wenyewe na zitawakomboa kutoka katika dimbwi la umaskini ambapo mpango huo utakuwa endelevu mpaka atakapokoma kuwa mbunge wa jimbo hilo. "Ni imani yangu kwamba kupitia mpango huu vijana wengi katika jimbo letu wataweza kujiajiri wenyewe na hili ni zoezi la kudumu, leo hii tumepokea pikipiki 20, lakini kutokana na asilimia 30 itakayolipwa na wakopaji wa mwanzo, tutaongeza pikipiki sita na hizo sita zitaleta pikipiki nyingine mbili," alisema

No comments:

Post a Comment