Na Andrew Ignas
UO N G O Z I w a
U m o j a wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kata ya Tandika wilayani
Temeke, Dar es Salaam umesema umechoshwa na mwenendo wa chama kutowapa
kipaumbele baada ya uchaguzi.
Hayo yalisemwa juzi na Kamanda wa vijana
wa UVCCM katika kata hiyo ambaye pia ni Katibu wa CCM Wilaya ya Kisarawe, Zena
Mgaya wakati wa kufunga Baraza Maalumu la Vijana Kata ya Tandika.
Baraza ambalo liliambatana uzinduzi wa
mashina ya UVCCM Kilimani na Sateta ambayo yalizinduliwa na Mwenyekiti wa UVCCM
Mkoa wa Dar es Salaam, Omari Matulanga.
"Hili lipo wazi, sasa nasema ni
mwisho kama wanachukulia sisi ni kama watu tunawanadia sera zao ili wachukue
nchi basi imefikia mwisho, tumechoshwa," alisema Zena Mgaya.
No comments:
Post a Comment