30 July 2013

TUCTA YAPINGA VIWANGO VIPYA VYA MISHAHARA



Grace Ndossa na Goodluck Hongo

SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), limeshangazwa na viwango vipya vya mishahara ambavyo vimetangazwa na Serikali na kwamba ni kinyume na jinsi pande mbili hizo zilivyokubaliana awali
.Akizungumza na Majira Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TUCTA Nicholous Mgaya, alisema ingawa hajapata waraka huo, lakini viwango hivyo ameviona kupitia kwenye vyombo vya habari na kubaini kwamba, hivyo sivyo walivyokubaliana na Serikali.

Kutokana na hali hiyo, alisema tayari ameiandikia barua Serikali kuomba waraka huo wa viwango vya mishahara ili kuona vimeongezeka kwa kiwango gani.Alisema viwango vilivyotolewa ambavyo ameona kwenye vyombo vya habari vimeongezeka kwa silimia 8 tu kati ya asilimia 40 walizokuwa wamekubaliana na Serikali.

Mgaya, alisema wamekuwa wakikaa na Serikali na kujadili viwango vya mishahara, lakini Serikali wamekuwa si waaminifu kutekeleza makubalino yao na vyama vya wafanyakazi.

“Nimeshangazwa na viwango hivyo vipya vya mishahara kwani havikidhi matakwa ya wafanyakazi na ni kinyume na matarajio ya makubaliano yao na serikali,” alisema Mgaya.

Alisema walikubaliana viwango vipya vya mishahara viwe ni kuanzia asilimia 20 na 40 kwa kima cha chini, lakini Serikali imetekeleza asilimia nane tu ya makubaliano yao.

Alisema kuwa viwango vya ulipaji kodi vimepanda, zikiwemo kodi za vinywaji, kadi za simu, huduma za pesa kwenye mitandao ya simu zimeongezeka, hivyo kiwango kilichoongezwa kwenye mishahara hakimpi unafuu mfanyakazi.

Mgaya alisema viwango hivyo vipya vimelenga tu watumishi wenye mishahara ya chini, lakini kwa wenye mishahara mikubwa k iwa n g o k i l i c h o o n g e z e k a hakilingani kwani kimeongezeka kidogo sana.

Naye Profesa, Mwesiga Baregu Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha St Augustine, alisema kiwango hicho cha mshahara hanikidhi matakwa ya wafanyakazi kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha.

Alisema wafanyakazi tayari walipendekeza kiwango cha mishahara kima cha chini kiwe ni sh 300,000, lakini kiwango hicho walichoongeza hakiwezi k u t o s h e l e z a ma h i t a j i y a wafanyakazi.

Pia alisema Serikali ilitakiwa kuangalia kigezo kikuu cha kupanda kwa gharama za maisha ndiyo iweze kuangalia itaongezaje viwango vipya vya mishahara ili kumpunguzia mwananchi mzigo.

“Kiwango cha mishara kilitakiwa kuanzia sh 300,000 ndiyo inayoweza kukidhi mahitaji ya mfanyakazi ili aweze kumudu gharama za maisha,”alisema Profesa Baregu. Kiwango cha chini kimepanda kutoka sh 170,000 hadi sh 240,000

No comments:

Post a Comment