30 July 2013

MAMIA WAJITOKEZA KUMUENZI WANGWE



 Na Thomas Itembe,Tarime

MAMIA ya wananchi Wilayani Tarime jana wamejitokeza kuhudhuria kumbukumbu ya kumuenzi aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Wilaya Tarime, maheremu Chacha Wangwe
.Kumbukumbu ya kumuenzi marehemu Wangwe ilianzishwa na aliyekuwa Diwani wa Kata ya Sabasaba, John Heche, baada ya kufariki kwa ajali ya gari Julai, 2007 akiwa safarini kutoka Dodoma kwenda jijini Dar-es Salaam.

Katika kumbukumbu hiyo wa n a n c h i wa Ta r ime n a Tanzania kwa ujumla walitakiwa kumkumbuka na kumuenzi kwa sababu alikuwa shujaa asiyeogopa na mtetezi wa wanyonge wakati wa uhai wake.

Akizungumza wakati wa kumbukumbu hiyo, Heche alisema, marehemu Wangwe hakukubaliana alikuwa mtetezi wa akinamama wauza mboga na matunda, ambapo alipinga ushuru waliokuwa wakitozwa hadi ukazuiwa na mahakama.

Heche alitumia nafasi hiyo kuwataka vijana wa CHADEMA kuacha malumbano ndani ya chama badala yake wajenge nguvu ya pamoja kuimarisha chama kama hali aliyokuwa nayo, marehemu Wangwe na kuwa wapinzani wao ni CCM si viongozi ndani ya chama.  

.

No comments:

Post a Comment