BARAZA la Taifa la uwezeshaji Wa n a n c h i Ki u c h umi
(NEEC),limewafadhili zaidi ya wafanyabiashara wadogo wadogo 50 kushiriki katika
maonyesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, anaripoti Rehema Maigala.
Afisa
Mwandamizi wa Uwezeshaji wa NEEC, Edward Kessy alisema jana kuwa mwaka huu
wamefadhili makundi ya seremala, ushonaji, usindikaji vyakula, ufumaji na wale
wanaoongeza thamani bidhaa zao lengo ikiwa ni kuwawezesha kupata masoko.
Al i s ema mi o
n g o n i mwa wajasiriamali hao wako wanaotoka mikoa yaa Mbeya, Mtwara na
Kibaha wakiwa na bidhaa za aina mbalimbali zinazotengenezwa na kampuni za
kizalendo.
"Hapa
wanaonyesha bidhaa mbalimbali wanazotengeneza na teknolojia wanazotumia katika
kutengeneza, NEEC inaona hii ni fursa kwao kupata mbinu za kutafuta masoko na
namna ya kuboresha bidhaa zao ili wakamate masomo ya kimataifa," alisema.
Alisema hata ushindi walioupata mwaka jana
ulitokana na jitihada kubwa walizofanya kuwawezesha wajasiriamali wa kada
mbalimbali kushiriki maonyesho na katika kuanzisha miradi mbalimbali.
Alisema huu ni mwaka wa tatu mfululizo
wanawawezesha wajasiriAmali kushiriki maonyesho hayo kwa lengo la kuwafungulia
masomo ya ndani na nje ya nchi.
"Wajasiriamali kuja hapa wenyewe inakuwa ngumu
kutokana na gharama sasa, kila mwaka NEEC tunatarajia kuwezesha wajasiriamali
zaidi kuja hapa kwa ajili ya kuonyesha bidhaa zao itawapa fursa nzuri
kibiashara," alisema.
No comments:
Post a Comment