30 July 2013

TATA YAKABIDHI MAGARI 30 KWA UDA


KAMPUNI ya TATA African Ho l d i n g s ( Ta n z a n i a ) L t d inayojishughulisha na uuzaji wa magari imekabidhi magazi zaidi ya 30 kwa Kampuni ya Usafirishaji jijini Dar es Salaam (UDA) kwa lengo la kupunguza tatizo la usafiri, anaripoti Benard Bugoma
Akikabidhi magari hayo hivi karibuni kwa UDA Meneja Biashara wa kampuni ya TATA Bw.Divyesh Ramanandi alisema kati ya magari hayo 15 yana uwezo ya kubeba abiria 40 kwa mkupuo mmoja kwa kila basi."Mabasi hayo ni makubwa ukilinganisha na daladala zinazotoa huduma jijini hapa kwani yana uwezo wa kuchukua abiria 40 waliokaa katika siti kwa mara moja, na nina uhakika ni imara kwani yana uwezo wa kudumu kwa muda," alisema Bw.Ramanandi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa UDA Bw. Hamidy alitoa wito kwa wananchi wa jiji hilo kuyajali magari hayo na kuuona mradi huo kama ni wao kwani kampuni hiyo haipo kibiashara bali kuwasaidia wakazi hao."Naomba kila mmoja awe mlinzi awapo kwenye basi, msisite kumbainisha mtu yeyote utakayemuona kwa makusudi anafanya uharibifu wa namna yoyote ile ndani ya basi," alisema Bw. Hamidy.

No comments:

Post a Comment