David John na Penina
Malundo
SHIRIKA
la Umeme Tanzania (TANESCO) limekutana na shirikisho la Chama cha Wamiliki wa
Viwanda nchini (CTI) kwa lengo la kuzungumzia mikakati kabambe ya kumaliza
tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara hasa katika viwanda.Mkutano huo
uliohudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Felshers Mramba Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki katika ofisi za shirika hilo ambapo aliwaambia
wanachama hao kuwa Shirika la Umeme limekuwa likipambana na kuimarisha
upatikanaji wa huduma ya umeme wa uhakika nchini.
Alisema Shirika linatambua fika matatizo yanayojitokeza katika kupata umeme wa uhakika nchini hasa katika Mkoa wa Dar es Salaam hivyo ili kuhakikisha tatizo hilo linapata ufumbuzi wa kuongeza upatikanaji wa vituo vitano vitakavyo fanya kazi ya kusambaza umeme katika Mkoa wa Dar es Salaam."Shirika linatambua fika changamoto kubwa iliyopo kuhusu umeme ndiyo maana Serikali kupitia TANESCO wameweza kuingia mikataba mingi ya kuanzisha vituo mbalimbali vya kuzalisha umeme ili kuwezesha huduma hiyo kupatika kwa uhakika," alisema.
Alisema tayari
mpaka sasa vituo zaidi ya vitano vipo katika ujenzi wa kuwezesha kusambaza na
kuponza umeme katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam,vituo hivyo ni
pamoja na Mbagala,Gongo la mboto, Kurasini, Kinyerezi, pamoja na katika ya jiji
hivyo kuna uhakika baada ya ujenzi huo tatizo la umeme litakuwa limepatiwa
ufumbuzi.
Aliongeza kuwa
mbali na vituo hivyo ambavyo vipo Dar es Salaam lakini Serikali imeweza kuingia
mikataba mikubwa ya upatikanaji wa huduma ya umeme Tanzania ,ambapo pia huduma
hiyo itaunganishwa hata kwa baadhi ya nchi jirani kama Nairobi, Ethiopia Zambia
na itapita katika Mikoa wa Mtwara.Aliitaja mikoa mingine ni pamoja
Singida,Mbeya, Shinyanga, Somanga , Arusha na Mikoa ya North West Grid ambayo
ni Geita, Kahama, Nyakanyanzi na Kigoma.
Pia aliwaambia wadau hao kuwa Shirika
linatambua hasara mbalimbali inayojitokeza pindi matatizo ya umeme yanapotokea,
lakini aliwahakikishia kuwa ongezeko la vituo hivyo hasa katika jiji la Dar es
Salaam litawezesha kuimarisha upatikana wa umeme katika viwanda na sehemu
nyinginezo.
"Tunajua kuwa Shirika la TANESCO
kwa asilimia 60 linategemea kuongeza pato lake kupitia viwanda hivyo nasi
hatuwezi kuwaangusha kwani tunatambua kuwa nyie ni wateja wetu wa kubwa.na ili
kuhakikisha hampati hasara ya kuharibika kwa vifaa vyenu pindi matatizo ya
umeme yanapojitokeza,tumejipanga kuleta hu dumayamr adiwakud hibiti nakutoa taa
r ifakwa wa katikamakunakuwanatatizololote la umeme."alis ema Mramb a.
Katika hatua nyingine Shirika
hiloli mes ema limeku tananawada uwaKampuni zasimu za mkononi ilik ujadilin
amnashi rika linavyoweza kutumi ahudu mazaombalimbali kwaku
toataarifazamabadili yaumem ekwa wanan chi wake ,ambapom udaw owote wateja wotewataanza
kupat ataarifakupitiasimu zao za mkononi.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa CTI, Felix
Mosha alisema wanachama wake wanaona mabadiliko makubwa ya kuridhisha shirika
hilo ukilinganisha miaka michache ya nyuma, hivyo ni matumaini kuwa uboreshwaji
huo uwe na ubora na uhakika zaidi.
"Tunachoweza kusema ni kwamba TANESCO imekuwa ni mpya na endapo
mtakapokuwa mnakwamishwa na fedha basi msisite kutuambia mapema ili nasi tuweze
kuona namna ya kuweza kulisaidia shirika,"alisema Mosha.
No comments:
Post a Comment