29 July 2013

MAUGO,MWAKYEMBE WACHEZEA VICHAPO URUSI



Na Rajabu Mhamila
BONDIA Mada Maugo, mwishoni mwa wiki amechezea kichapo kutoka kwa bondia Movsur Yusupov wa Urusia katika pambano la raundi nane huku bondia wa Tanzania akipigwa kwa TKO ya raundi tano.Mchezo huo ulifanyika katika viwanja vya Trade And Entertainment Centre (Moskva), Kaspiysk nchini Urusi.
Baada ya kupoteza mchezo huo, bondia huyo atapanda tena ulingoni Agosti 30, mwaka huu na Thomasi Mashali kutafuta ubingwa wa WBF Africa uzito wa kati mpambano utakaokuwa wa raundi 12.Naye bondia Benson Mwakyembe ambaye pia yupo nchini humo alikubali kichapo cha KO raundi ya saba, katika pambano la raundi ya 7 katika mpambano wa raundi 8. Mabondia hao wa Tanzania walionesha kuwa na viwango vya kutosha, ila walizidiwa ufundi na maarifa ya mchezo huo ulingoni.Hata hivyo, mapambano hayo yalikuwa si ya kutafuta ubingwa wowote isipokuwa kuwapa uzoefu mabondia hao wa Tanzania. Akizungumzia kuhusu mabondia wa Tanzania juzi, Rais wa TPBO, Yasin Abdallah 'Ustaadhi' alisema kwamba wamepanga mikakati ya kutafuta mapambano katika nchi za Kusini mwa Afrika.Alisema mara nyingi mabondia wa Tanzania wamekuwa wakipigana na wenzao wa Kenya na Uganda, ambao wamekuwa si wazuri kwani Watanzania wamekuwa wakishinda kila wanapocheza na mabondia wenzao wa Afrika Mashariki. "Sasa hivi tunataka kuhamia Zambia, Namibia na hata Afrika Kusini kwa kuwa Kenya na Uganda hakuna mabondia wazuri wamekuwa wakipigwa kila mara na mabondia wetu," alisema Ustaadhi

No comments:

Post a Comment