25 July 2013

SERIKALI YAZIANGUKIA ASIZE



 Na Lilian Justice, Morogoro
.SERIKALI mkoani M o r o g o r o imeziangukia Asasi za kiraia mkoani humo ikizitaka kuelekeza nguvu zake katika kutekeleza vipaumbele vitano vya kitaifa na vilivyoelekezwa na Serikali ili kuinua mkoa na taifa .Hayo yamefahamika mwishoni mwa wiki kwenye mkutano wa Katibu tawala mkoa huo, Elia Ntandu alipokutana na baadhi ya viongozi wa asasi hizo mkoani humo na kuwaeleza dhamira yake ikiwemo kutambuana kwa kupeana taarifa fupi yenye historia, kazi zilizofanywa na asasi husika na mipango yake ya baadae.

"Mbali na kufahamiana nimewaita niwape dira na vipaumbele vya Serikali katika kuinua uchumi na kuukabili umaskini, sasa vipaumbele vya Taifa ni vitano ikiwemo kukuza sekta ya kilimo, maji, nishari, elimu na mawasiliano na kimsingi Morogoro imepewa dhamana ya kuzalisha mchele na sukari katika kiwango cha kutosheleza mahitaji ya nchi," alisema Ntandu.Akifafanua juu ya azma yake Katibu Tawala huyo wa mkoa alisema angependa kuifahamu kila asasi inachokifanya kwa jamii ili wapeane majukumu na kujiwekewa utaratibu utakao wezesha dira ya serikali kutekelezeka kwa wakati na kwa faida ya watu wote kama ilivyo kwenye dhamira za asasi hizo na serikali kuu.
"Labda kwa namna moja au nyingine niseme mpango wa ushirikiano kati ya sekta ya umma, yaani serikali, na sekta binafsi imeonyesha kuleta mafanikio makubwa ya maendeleo kwa jamii na kupitia mpango huu mimi nimeamua kuanza na ninyi ili tujipange twende vipi..., sijui naeleweka jamni," alifafanua zaidi.
Hata hivyo alipowataka kutoa changamoto na nini kifanyike baadhi ya wajumbe wa mkutano huo waliirushia lawama Serikali katika ngazi zote kutotoa ushirikiano kwa asasi hizo na kuanzisha uhasama kati yake na asasi hizo kwa kilichodaiwa kuhisiwa ni vibaraka wa vyama vya siasa.
"Kuna changamoto nyingi lakini leo tukutajie chache mfano hakuna uhusiano wa karibu kati ya watumishi wa umma na sekta hii binafsi, tunapata vitisho hata vya kuuawa, taarifa zetu zinafichwa baada ya tafiti na wengine tunatajwa kuwa wafuasi wa vyama vya siasa..., hii ni hatari kuu," alisema Charles Mengele.
Aidha kwa upande wake Katibu wa umoja wa asasi hizo mkoa, Iddi Mdanku alisema mbali na changamoto zinazozikabili asasi hizo zimewezesha kukabili changamoto zilizo katika jamii na kuharakisha maendeleo katika baadhi ya sekta na jamii.
Mdanku alisema kutokana na mpishano wa kimawazo wamejikuta wakifanya kazi kwa kupishana na kusababisha kuonekana kama za kichonganishi kutokana na watendaji wengi serikalini kufanya kazi kwa mazoea.
Hata hivyo katika mkutano huo walikubaliana kuunda timu itakayowakutanisha mara kwa mara kuboresha utumishi, watumishi wa umma uwajibikaji kwa mujibu wa sheri, kuwekwa ukurasa wa asasi kwenye tovuti ya mkoa, asasi wilayani kuandaa wawakilishi na agizo la Rais wazee kufutiwa kodi na huduma bure litekelezwe

No comments:

Post a Comment