25 July 2013

TAKUKURU YAWABURUTA KORTINI VIGOGO WATATU


Na Israel Mwaisaka, Kyela 
WATU watatu akiwemo wakala wa pembejeo za kilimo katika Kata ya Ngonga wilayani Kyela, Geofrey Wanyato wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya Kyela na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakikabiliwa na makosa 16 ya rushwa

A k i w a s ome a ma s h t a k a watuhumiwa hao mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo ya Wilaya, Joseph Luambano na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Joseph Mlebya alisema kuwa mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa ni wakala na wenzie wawili ambao ni Steven Mwaipaja ambaye alikuwa ni ofisa mtendaji wa kijiji cha Ngonga na Alex Mbanganile mwenyekiti wa kamati ya vocha ya kijiji wote walikula njama na kuiibia halmashauri ya wilaya sh milioni 4.6
Alisema kuwa mtuhumiwa wa kwanza ambaye alikuwa ni wakala wa pembejeo katika mwaka wa 2011-12 alighushi nyaraka ambazo ni vocha na fomu za wakulima na kumwibia mwajiri wake ambaye ni Halmashauri ya Wilaya ya Kyela na kufanikiwa kumwibia sh milioni 4.6 na kuiingizia hasara kubwa halmashauri ya wilaya.
Ambapo ofisa mtendaji wa kijiji na mwenyekiti wa kamati ya vocha ya wilaya wao walimsaidia mtuhumiwa kutenda kosa hilo na kumwezesha kujipatia fedha hizo hivyo wote kwa pamoja ni wakosaji na wametenda kosa la jinai
Mwendesha mashtaka huyo wa TAKUKURU a l i i e l e z a mahakama hiyo kuwa makosa mengi yanafanana ila yamekuwa yakijirudia kwa tarehe tofauti hadi kufikia makosa 16 ambayo yameisababishia halmashauri ya wilaya hasara kubwa lakini pia kuwanyima haki yao wakazi wa Ngonga ambao ni wakulima kushindwa kupata pembejeo za kilimo
Washtakiwa wote kwa pamoja wamekana mashtaka yao yote na wapo nje kwa dhamana hadi hapo kesi yao itakapotajwa Agosti 22 mwaka huu

No comments:

Post a Comment