24 July 2013

SALAMU ZAMIMINIKA KWA MTOTO WA KIFALME LONDON, Uingereza
SALAMU z a p o n g e z i zimekuwa zikimiminika kutoka pande zote za dunia kusherehekea kuzaliwa kwa mtoto wa kiume wa Prince William na mkewe Kate. Mtoto huyo anakuwa wa tatu katika orodha ya kurithi kiti cha ufalme.Maelfu ya watu waliokuwa wakiwatakia mema walimiminika katika jumba la kifalme la Buckingham baada ya taarifa hizo kuvuja.

Uzazi huo wa kifalme baadaye unatarajiwa kupewa heshima kwa milio ya bunduki na kupigwa kengele za Westminster Abbey. Prince William alikuwepo katika Hospitali ya Mt. Mary, Magharibi mwa London, akisubiri na alishinda usiku na Catherine pamoja na mtoto huyo baada ya kuzaliwa. Msemaji wa Jumba la Kensington alisema ilikuwa "mapema mno" kusema kama wangeruhusiwa kutoka hospitali jana.
Wanandoa hao walitarajiwa kuongea na timu yao ya madaktari kabla ya uamuzi kufanyika.Kwa mujibu wa BBC, uwezekano haukuwa mkubwa kwa Malkia kumtembelea kitukuu chake hospitali, lakini iliongeza kusema; "bila shaka anaweza kumtembelea akiwa binafsi atakapoondoka hospitali". Baada ya taarifa ya kuwasili kwa mtoto huyo kutangazwa na jumba la kifalme la Kensington, umati mkubwa wa watu pamoja na waandishi wa habari ulishangilia nje ya hospitali.

No comments:

Post a Comment