- MMLIKI WAKE ADAIWA KUKODISHA BUNDUKI KWA MAJAMBAZI
- ANAYETAPELI KWA JINA LA MCHUNGAJI RWAKATARE MBARONI
Leah Daud na Josephine Burton
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam, limekamata kiwanda cha kutengeneza kienyeji bunduki za aina mbalimbali
maeneo ya Kawe, wilayani Kinondoni.Kiwanda hicho
kinadaiwa kumilikiwa na mkazi mmoja aliyetajwa kwa jina cha Charles Masunzu
(30). Akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kamishna wa Polisi, Kanda Maalum Dar es
Salaam, Ally Mlege, alisema baada ya kukamatwa kwa mmiliki huyo, aliwataja
majambazi ambao amekuwa akiwakodisha silaha zake kwa ajili ya kwenda kufanya
uhalifu.
Walitaja watu
hao kuwa ni Matola Rashid (27), Omary Hassan (43), Martha Mhagama(32) na
Mwasiti Maulid (22).Alisema
watuhumiwa hao walikamatwa na bunduki aina ya SMG iliyosajiliwa kwa namba 02704
ikiwa na risasi 20 ambapo ilikuwa imekatwa kitako. Alisema
majambazi hao baada ya kuhojiwa walikiri kujihusisha na matukio ya uporaji
sehemu mbalimbali za jijini Dar es Salaam kwa kutumia silaha. Alisema kwamba
majambazi hao walikiri kumpora silaha Polisi Wilayani Rufiji akiwa anasindikiza
magari kutoka Ikwiriri Mkoa wa Pwani mwaka 2007.
Alisema mtuhumiwa anayedaiwa kumiliki
kiwanda cha silaha alipopekuliwa alikutwa akimili bunduki mbalimbali, ikiwemo
SMG namba 2539 Double Bore. Rifle tatu, Fiffe Mark tatu, Rifle Mark 3 Pistol
KJW Works, mitutu mitano iliyotengenezwa kienyeji, pingu, risasi 36, maganda 17
ya risasi, mkebe wa gololi za silaha aina ya SMG na mifuko ya kuhifadhia
silaha.Pia alisema mtu huyo alikamatwa pia na
vifaa vingine vikiwemo vya kutengenezea silaha za kienyeji, mikasi minne aina
tofauti na mipini mitatu ya silaha aina ya Rifle. Pia mtu huyo pia alikamatwa
na vifaa vingine vya aina mbambali.
Katika tukio lingine,
Jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata mtu mmoja, Mfaume Omary maarufu kwa jina
la Mau (29) anayetumia majina ya viongozi wa Serikali, dini na watu maarufu na
kujipatia fedha kwa kuvaa uhusika wa mtu husika.
Alisema kwa hivi karibuni wamekuwa
wakifuatilia nyendo zake baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mchungaji Getrude
Rwakatare, kuwa jina lake linatumiwa vibaya na watu ili kujipatia fedha.
Mlege alisema jeshi la Polisi wa l i f
a n i k iwa k umk ama t a mtuhumiwa huyo akiwa anamiliki simu namba 0659 736454
ikiwa imesajiliwa kwa jina la Mfaume Said Omary na 0659 164744 ikiwa
imesajiliwa kwa jina la Alex Mtenga.
Alisema baada ya mahojiano na mtuhumiwa
alikiri kutapeli watu mbalimbali wakiwemo wachezaji maarufu wa timu za mpira
hapa nchini kwa kuvaa uhusika wao.
Hata hivyo alisema mtuhumiwa huyo
anaendelea kushikiliwa kwa mahojiano na atafikishwa Mahakamani baada ushahidi
kukamilika.Wakati huo huo, Kamishna Mlege alisema Polisi wanamsaka mtu anayetuhumiwa kummwagia
tindikali Mkurugenzi wa Home
Shopping Center, Said
Mohamed Saad.
No comments:
Post a Comment