31 July 2013

PRO. MAJIMAREFU ATANGAZA KUJIUZULU



Na Mashaka Mhando, Korogwe  
MBUNGE wa Jimbo l a K o r o g w e , Stephen Ngonyani Profesa Majimarefu, amesema atakuwa tayari kujiuzulu nafasi yake ya ubunge endapo atashindwa kutekeleza ahadi zake zilizomo kwenye Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 hadi 2015. Akizungumza katika uwekaji wa jiwe la msingi la Kituo cha Polisi cha Tarafa ya Magoma lililokuwa likiwekwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni (Mstaafu) Chiku Gallawa, mbunge huyo alisema kuwa atakuwa tayari kujiuzulu endapo hatatekeleza ahadi zake na kwamba, kazi anazozifanya kila anapopata fursa za kutembelea jimbo hilo, amekuwa akitekeleza.
Mbunge huyo alianza kuanisha kazi mbalimbali ambazo amezifanya katika tarafa hiyo, ikiwemo kutoa bati 60 zenye thamani ya shilingi milioni 2.6 kwa ajili ya kuezekwa kwenye soko lililopo katika Kijiji cha Magoma, kiasi cha shilingi milioni 1 kwa ajili ya kusaidia shule ya Sekondari Magoma. 
Alimwambia mkuu huyo wa mkoa hata kukamilika kwa ujenzi wa jengo la mahakama ya mwanzo tarafa hiyo ya Magoma, ni matokeo yake ya kuibana Serikali hasa Waziri wa Sheria kuhakikisha Tarafa hiyo na Mkomazi zinajengewa mahakama ili kuondoa msongamano katika maeneo mengine. Linginealilomwambia Mkuu huyo wa mkoa mbunge huyo, alisema kuwa ni suala la umeme ambapo kwasasa wataalamu wa mpango wa uwekezaji umeme vijijini (REA), wanatandaza nguzo katika vijiji mbalimbali vya tarafa hiyo kama ambavyo amehakikishiwa na Waziri katika Bunge lililopita. " M h e s h i m i w a k a z i tunafanya huku katika jimbo hili, nitakuwa tayari kujiuzulu endapo ahadi nilizozitoa zitazitekeleza lakini naamini kwa ushirikiano na wananchi hawa nitatekeleza ili mwaka 2015 chama chetu cha CCM tutembee kifua mbele," alisema mbunge huyo. Mbunge huyo alisema atashauriana na watendaji na viongozi wa Serikali ili bati 60 alizozitoa kwa ajili ya soko hilo, zibadilishwe matumizi na sasa bati hizo zipangwe kuezekea kituo hicho cha polisi kisha halmashauri watakapokuwa tayari kulijenga soko hilo, atatoa bati nyingine

No comments:

Post a Comment