Na Mwandishi Wetu, Ngara
BODI ya Huduma za Maktaba Tanzania
(TLSB), imetoa vitabu 3,240 vyenye thamani ya sh.milioni 54.3 kwa ajili ya
kuanzisha maktaba mbili za Wilaya ya Ngara, mkoani Kagera.Mkurugenzi Mkuu wa TLSB, Dkt. Alli
Mcharazo, alisema hayo jana mara baada ya kuzinduliwa kwa Maktaba ya Wilaya ya
Ngara na ile ya tarafa ya Rulenge
. Katika taarifa yake kwa vyombo vya
habari, Dkt.Mcharazo alisema maktaba hizo zitakazokuwa zikiendeshwa na TLSB kwa
kushirikiana na halmashauri ya wilaya zitasaidia kuleta maendeleo kwa jamii
hiyo wakiwemo wanafunzi.Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, maktaba
ya Ngara ilipewa vitabu 2,018 vyenye thamani ya Sh.milioni 36.9 na ile ya
Rulenge ilipata vitabu 1,222 vyenye thamani ya sh.milioni 17.3.
Mcharazo alisema pia bodi hiyo imetoa
wakutubi wawili ambao watagawanywa katika maktaba hizo kwa ajili ya
kuzisimamia."Tunafurahi kwamba wananchi wa
Wilaya ya Ngara sasa wanaanza kupata huduma za maktaba ili kujifunza masuala
mbalimbali yatakayowasaidia katika kuleta ma e n d e l e o y a o , " a l i
s ema Mcharazo. Alisema hadi sasa bodi hiyo ina maktaba
katika mikoa 21, wilaya 19 na tarafa 2 na kwamba juhudi zinafanyika kueneza
huduma hiyo katika maeneo yaliyobaki hasa vijijini.
Akizindua maktaba hizo, Mbunge wa Jimbo
la Ngara, Deogratias Ntukamazina alisema wilaya hiyo imebahatika kuzindua
maktaba mbili kwa wakati mmoja."Ni tukio tulilolisubiri kwa muda
mrefu, jamii ya Ngara itapata maarifa kupitia maktaba hizo na hivyo kujiletea
maendeleo yao," alisema Ntukamazina.
Aliwataka wananchi wakiwemo wanafunzi kujitokeza
kuzitumia maktaba hizo ili kujiongezea uelewa
No comments:
Post a Comment