30 July 2013

NAIBU WAZIRI AGEUKA MBOGO



Na Martha Fataely, Mwanga
NAIBU Waziri wa Maji, Dkt. Binilith Mahenge ameagiza mamlaka ya majisafi ya Wilaya ya Mwanga ifanyiwe ukaguzi wa matumizi ya kuanzia mwaka 2010 baada ya kujiendesha bila bodi ya uendeshaji.Dkt. Mahenge ametoa agizo hilo baada ya kusomewa taarifa na Meneja wa mamlaka hiyo, Stephen Albinus ambayo imeonesha upungufu mkubwa
. Baada ya kutoridhishwa na taarifa hiyo Naibu Waziri amempa miezi mitatu meneja huyo kuwa chini ya uangalizi wa halmashauri ya wilaya ambayo ndiyo mwajiri wake.Alisema utendaji mbovu wa meneja huyo umesababishwa na kujiona hawajibiki kwa halmashauri hiyo jambo ambalo ni kubwa.
Kwa upande wake meneja huyo wa Mamlaka ya Maji Mwanga alisema kwa muda wote amekuwa akijitambua kama anawajibika kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) na kutuma taarifa zake kwa taasisi hiyo.Kutokana na hali hiyo Dkt. Mahenge ameitaka halmashauri ya wilaya hiyo isiporidhika na utendaji wa meneja huyo kwa miezi mitatu imuondoe na wizara italeta mtaalamu mwingine. Aidha aliutaka Mkoa wa Kilimanjaro kuanza mchakato wa kuunda bodi ya mamlaka hiyo ili ifanye kazi kwa ufanisi na wizara itatoa ushirikiano.

No comments:

Post a Comment