Na Mosi Mrisho
MBIO za kuwania madaraka ndani ya
Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), zimeanza na zinatarajiwa kuhitimishwa
jijini Mwanza kesho ambapo uchaguzi huo utafanyika.
Akizunmgumza Dar es Salaam jana Afisa
Michezo Msaidizi wa BFT Richard Mganga, alisema mpaka sasa wamejitokeza watu
watano kuchukua fomu za kuwania uongozi ndani ya chama hicho.
Maganga alisema uchaguzi huo utafanyika
baada ya viongozi wa sasa kumaliza muda wao wa uongozi kwa mujibu wa katiba ya
chama hicho.
Alisema wapo watu wengi wanaohitaji
kuingia kwenye uongozi huo, lakini zipo sifa mbalimbali ambazo zinahitajika ili
kuweza kushiriki uchaguzi huo.
Maganga aliongeza kuwa wadau kabla ya
kufikiria kuingia BFT lazima wagombea wajichuje wenyewe, ambapo mgombea pamoja
na elimu yake au kuwa na sifa nyengine anatakiwa kuwa na sifa za uongozi
nauzoefu wakutosha.
Alisema mpaka sasa waliojitokeza kuchukua fomu za
kuomba uongozi ni watano.
No comments:
Post a Comment