Na Eliasa Ally, Iringa
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) , Mk o a wa Iringa imemfikisha mahakamani Mhandisi wa Idara ya Maji
wilayani Ludewa, Mkoa wa Njombe, Athanasius Munge kwa kumdanganya mwajiri wake
ambaye ni Mkurugenzi wa wilaya hiyo.
Udanganyifu huo unadaiwa unatokana na kumpelekea Mkurugenzi
(hakutajwa jina) wa halmashauri hiyo risiti za malipo hewa yenye zaidi ya sh.
milioni 21 kwa madai kuwa kuna wajumbe wa Idara ya Maji walikula na kunywa chai
wakati wanatembelea miradi ya maji katika wilaya hiyo.
Wajumbe hao walidaiwa walijipatia chakula hicho katika mgahawa wa
mfanyabiashara, Videa Kayombo mjini hapa ambaye anadaiwa kumpatia risiti feki
ili waweze kujipatia fedha hizo.
A k i s oma ma s h t a k a y a watuhumiwa hao jana, Mwendesha
Mashtaka wa TAKUKURU, Mkoa wa Iringa, PP Imani Mitume Mizizi kwa watuhumiwa hao
wawili mbele ya Hakimu Hassan Juma wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa alisema
watuhumiwa hao walifanya makosa ya kufoji risiti zao ili wajipatie malipo hayo.
Aidha, alidai katika makosa hayo Mhandisi Athanasius Munge
alipatikana na makosa matano ambapo makosa manne yanamhusu na kosa la tano
wameunganishwa na Videa Kayombo kwa kufoji risiti feki kwa nyakati tofauti za
sh. milioni 21.
Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, alisema kosa la kwanza kati ya
mwezi Oktoba 9 hadi 18 mwaka 2008 Mhandisi Munge alimpelekea risiti mwajiri
wake kumtaka alipe kiasi cha sh. milioni 4.2 kwa madai kuwa wajumbe wa Idara ya
Maji walifanya mkutano na kula chakula.
Sambamba na chai katika mgahawa wa Videa Kayombo; hivyo kukiuka
Sheria ya Manunuzi namba 11 ya mwaka 2007.
Aidha, alisema kosa la pili, Mhandisi Munge akiwa katika
Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Oktoba 7, 2008 alimpelekea mwajiri wake risiti
namba 0004994 iliyotolewa katika Mgahawa wa Merelendi unaomilikiwa na Videa
Kayombo akidai kulipwa sh. milioni 4.2 kwa madai kuwa wajumbe wa idara hiyo
walikula chakula na chai wakati si kweli.
Mwendesha
Mashtaka, Mzizi alisema kuwa kosa la tatu Oktoba 7, 2008 Mhandisi huyo
alimpelekea pia mwajiri wake vocha ya malipo namba 21 kutoka katika Mgahawa wa
Merelendi unaomilikiwa na Videa Kayombo kwa madai kuwa kamati ya wajumbe wa
maji kutoka vijiji vya wilaya ya Ludewa walikusanyika na kula chakula pamoja na
kunywa chai wakati si kweli na kumtaka Mkurugenzi kulipa malipo ya sh. milioni
4.2 kwa mwenye mgahawa huo.
Pia
Mwendesha mashtaka huyo alisema, katika kosa la nne Mhandisi Munge alilifanya
Oktoba 7, 2008 baada ya kumpelekea vocha feki ya malipo mwajiri wake namba 5/10
ambayo iliandikwa Oktoba 8, 2008 akidai kulipwa sh. milioni 4.2.
Alidai
kuwa, wajumbe wa Mradi wa Maji wa NRWSSP walikula na kunywa chai katika Mgahawa
wa Merelendi uliopo Ludewa ambao unamilikiwa na Videa Kayombo.
Mbali na
hayo alidai kuwa, katika kosa la tano linawaunganisha washtakiwa wote wawili
Mhandisi Munge na Videa Kayombo kwa kula njama za kuandaa hati feki za malipo
ya sh. milioni 4.2 kwa nyakati tofauti kuanzia Oktoba 9 hadi 18, 2008 kwa
kutaka kulipwa malipo ya fedha na Halmashauri ya Ludewa jumla ya sh. milioni 21
ambazo zilikuwa ni fedha hewa.
Katika kesi
hiyo, watuhumiwa wote wawili walikana mashtaka ya kutohusika na hujuma hizo
ambapo Mwendesha Mashtaka Mizizi alisema kuwa, upelelezi wa kesi hiyo
umekamilika ambapo alimwomba Hakimu tarehe ya kuanza kuisikiliza ikiwemo kuwaleta
mashahidi.
Hakimu Hassan Juma ambaye alikuwa anasikiliza kesi hiyo aliahirisha kesi
hiyo hadi Julai 15, mwaka huu ambapo watuhumiwa walirudishwa rumande baada ya
kukosa wadhamini ambao wangekidhi masharti
No comments:
Post a Comment