- ADAI WANAMSUMBUA USIKU AKIWA AMEALA NA MKE WAKE
- ASEMA HATA KWA MTUTU WA BUNDUKI HATATOA USHAHIDI
Na Moses
Mabula, Tabora
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Freeman Mbowe, amelitaka Jeshi la Polisi nchini kuacha mara moja
tabia ya kumsumbua usiku akiwa amelala na mkewe na kuanza kumlazimisha awapatie
ushahidi wa tukio la mlipuko wa bomu uliotokea kwenye mkutano wa kuhitimisha
kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani mkoani Arusha.
Mbowe alitoa kauli
hiyo juzi wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
kwenye viwanja vya chipukizi, mjini Tabora. Mkutano huo ulikuwa ni kwa ajili ya
kuimarisha chama hicho katika Kanda ya Magharibi.
Alisema kwamba, hivi
karibuni Polisi wakiwa na silaha walivamia nyumbani kwake usiku wa manane
wakidai wanatafuta ushahidi wa picha ya tukio la mlipuko wa bomu lililolipuka
mkoani Arusha katika kompyuta yake.
Alisema Jeshi la
Polisi kazi yake ni kuchunguza matukio, hivyo hata katika tukio hilo wafanye uchunguzi
wao wa kipolisi badala ya kukaa na kupoteza muda mwingi kutafuta ushahidi huo
kwake.
"Polisi
wamesomea uchunguzi sasa huku kwangu wanatafuta nini? Wao si wataalamu wa
kuchunguza matukio, sasa kwa nini wanashindwa kuchunguza hadi Mbowe awape
ushahidi?" alihoji na kuongeza;
" Mimi
hainiingii akilini hata kidogo, napata shaka
kama kweli kama walisomea uchunguzi."
Mbowe alisisitiza
kwamba hata kwa risasi hayupo tayari kutoa ushahidi huo kwa polisi hadi
Serikali itakapokubali hoja yake ya msingi ya kutaka iundwe tume huru ya kijaji
itabaini ukweli huo.
Katika hotuba yake
hiyo ambayo muda mwingi alitumia kuwashambulia polisi, alisema jeshi hilo limekuwa likifanya
kazi kwa maelekezo ya baadhi ya viongozi wa CCM ambao lengo lao ni
kuwakandamiza wananchi wanyonge.
Kuhusu Katiba Mpya
alisema kuwa mapendekezo ya kuwepo kwa Serikali tatu wananchi hawana budi
kuunga mkono hoja hiyo, kwani itakuwa mkombozi kwao.
Alisema muundo uliopo sasa wa serikali
mbili hauna masilahi kwa wananchi wa Tanzania Bara, kwani wamekuwa wakinyonywa
na wale wenzao wa Zanzibar.
Ka t i k a h a
t u a n y i n g i n e Mwenyekiti huyo wa CHADEMA taifa alimshambulia mbunge wa
jimbo la Tabora mjini, Ismail Aden Rage na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora,
Hassan Wakasuvi, kwamba wamekuwa wakichangia kwa kiasi kikubwa kuwadidimiza
wakulima wa tumbaku.
Mbowe alieleza kwamba wakulima
wa tumbaku mkoani Ta b o r a wa n a k a b i l iwa n a changamoto mbalimbali
zikiwemo viongozi wao kutowajali na madeni makubwa katika taasisi za fedha
yanayotokana na kutozwa riba kubwa kutoka kwenye mabenki. Alisema kuwa hali
hiyo imekuwa ikichangia mkulima huyo zao la tumbaku kushindwa kumudu maisha na
kubakia kuwa maskini.
Hao si uchunguzi wanatafuta kunachaziada wanataka
ReplyDeletechapa kazi kazi kaka mbele kwa mbele hakuna kulala hadi kieleweke
ReplyDelete