N a A n n a N k i n d a , (MAELEZO)
WA T A N Z A N I A wametakiwa kujifunza kuthamini vitu vya kwao na kuona
kuwa ni bora zaidi kwa kufanya hivyo hata wageni watavipenda kwani bidhaa
zinazozalishwa ndani ya nchi hazitapandishwa thamani na watu kutoka nje.
Mwito huo
umetolewa juzi na mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na waandishi
wa habari mara baada ya kumaliza kutembelea maonesho ya 37 ya Biashara ya
Kimataifa yanayofanyika katika uwanja wa Mwalimu Nyerere uliopo Barabara ya
Kilwa
wilayani Temeke
jijini Dar es Salaam.
Mama Kikwete
aliambatana na mke wa Mfalme Mswati wa Swaziland Inkhosikati Lambikiza, mke wa
Makamu wa Rais wa Zambia, Mama Charlotte Scott na Mwakilishi wa mke wa Rais
Joseph Kabila wa Jamhuri ya Watu wa Congo ambaye ni Waziri wa Jinsia, Watoto na
Familia Inagosi Bulo.
Mama Kikwete
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), alisema
kuwa, walitembelea maonyesho hayo ili kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa
ndani na nje ya nchi kuanzia ngazi ya juu hadi chini.
"Tumeona bidhaa za aina mbalimbali
zinazozalishwa ndani na nje ya nchi na jinsi watu wanavyoweza kubadilishana
uzoefu wa biashara hakika kadri siku zinavyozidi kwenda kuna maboresho makubwa
juu ya utengenezaji wa bidhaa zinazozalishwa nchini," alisema Mama
Kikwete.
Al iwa s h u k u r u wa g e n i
alioambatana nao kwa kuzipenda bidhaa zilizopo kwenye mabanda ya Watanzania na
kuwaomba wananchi kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Mkoa wa Dar es
Salaam kutembelea maonyesho hayo kwani kuona ni kujifunza.
P i a a l iwa p o n g e z a
n a kuwashukuru wanawake kwa kazi kubwa wanazozifanya za kuzalisha bidhaa na
kufanya biashara mbalimbali ambazo zimewasaidia kujiletea maendeleo yao na
jamii inayowazunguka.
No comments:
Post a Comment