MAGARI
saba ya aina mbalimbali yameteketea baada ya moto mkubwa kulipuka katika nyumba
eneo la Majumba Sita karibu na gereji bubu Wilaya ya Ilala jijini Dar es
Salaam.Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Wilaya ya Ilala,
Marietha Minangi alisema kuwa tukio hilo
lilitokea Julai 25, mwaka huu majira ya saa 08:00 usiku.
Kamanda huyo alisema, moto huo
ulilipuka katika nyumba yenye vyumba nane ya Kasim Nyoni (36) ambaye ni fundi
umeme na kuunguza magari hayo na mali nyingine.
Alisema kuwa, magari hayo
yalikuwa ya wateja katika gereji bubu inayomilikiwa na Azizi Abdalah (35)
ambapo moto huo ulianzia kwenye chumba cha duka na hatimaye kuenea ambapo
ulizimwa na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji cha Jiji.Kamanda huyo alisema, chanzo cha
moto hakijajulikana na upelelezi unaendelea.
No comments:
Post a Comment