MA M I L I O N I ya Watanzania wataathirika na
u a m u z i wa serikali kutoza kila mtumiaji wa simu
sh. 1,000 kwa mwezi kama kodi ya forodha, anaripoti Penina Malundo.
Hatua hii inatokana na mabadiliko ya muswada wa kodi
wa mwaka 2013 uliopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika
kikao cha bajeti kilichokwisha wiki iliyopita yamepitisha muswada huo kuanza
kutumika kuanzia Julai mosi, mwaka huu.
Kwa mujibu wa Chama cha makampuni ya simu za mkononi,
(MOAT) hatua hii itawazuia Watanzania wapatao milioni 8 ambao matumizi yao ya
simu hayafikii sh.1,000 kwa mwezi.
Chini ya sheria hii mpya ya kodi, makampuni hayo
yatalazimika kuwakata wateja wao wote sh.1000 kwa
mwezi na kuzikusanya kwa niaba ya serikali.
ìZaidi ya watumiaji wa simu milioni 8 nchini
wataathirika kutokana na ongezeko hilo la kodi mpya ya Shilingi 1,000. Tanzania
ina watumiaji wa simu za mkononi wapatao milioni 22 ambao ni sawa na asilimia
48 ya watumiaji wote wa simu,î taarifa hiyo ya MOAT imeeleza.
ìIwapo kuna watumiaji mi l i o n i 8 kwa s a s a
wanaotumia huduma ya mawasiliano ya simu za mikononi itakuwa ni vigumu kwa
wateja wengine wapya kuunganishwa na huduma za simu hasa walioko katika maeneo
ya vijijini.
Taarifa hiyo ya MOAT imeeleza kuwa inatambua jitihada
za serikali katika kukusanya kodi kwa ajili ya mipango ya maendeleo kwa
wananchi, hata hivyo
MOAT imebainisha kuwa kuanzishwa kwa kodi hiyo
kunakinzana na juhudi za kuwapunguzia mizigo ya kodi wananchi wenye kipato cha
chini.
MOAT imebainisha kuwa zoezi hili la kodi mpya ya
1,000/- itadhoofisha mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya mawasiliano ya
simu ambapo tumeshuhudia huduma hizi zikizidi kuwa nafuu kwa watu wote,î na
kuzorotesha mpango wa kimataifa wa Universal Communications Services Access
Fund (UCSAF), wa kuwezesha mawasiliano nafuu kwa wote.
MOAT imeiomba
serikali kufikiria upya juu ya tozo ya kodi hiyo mpya ya Sh. 1,000 ili kuweza
kufanikisha ukuaji wa matumizi ya mawasiliano ya simu kwa Watanzania wote.
No comments:
Post a Comment