03 July 2013

KAMPUNI ZA SIMU ZATAKIWA KURAHISISHA UPATIKANAJI TAARIFA KWA WAKULIMA


 SHIRIKA lisilo la kiserikali, Financial Sector Deepening Trust (FSDT) limesema kuwa kampuni za simu nchini bado zina nafasi kubwa kuhakikisha kuwa sekta ya kilimo inakua kupitia ubunifu wanaoweza kuufanya, anaripoti Christina Mokimirya.
Mkurugenzi wa musuala ya ufundi, FSDT, Bw. Sosthenes Kewe aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuwa kupitia ubunifu, kampuni hizo za simu zinaweza kusaidia urahisi wa upatikanaji taarifa mbalimbali kwa wakulima na wadau wengine wa kilimo.

Hi v i k a r i b u n i , k amp u n i mbalimbali za simu za mikononi zilizindua huduma kupitia mitandao yake ambapo wakulima watapata taarifa mbalimbali kuhusu shughuli za kilimo.
Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel kwa ushirikiano na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika na kampuni ya Sibesonke Limited zilizindua huduma za simu kupitia mtandao huo ambapo wakulima wataweza kupata taarifa kwa urahisi na kwa wakati kuhusu njia bora na za kisasa za kilimo kupitia huduma inayojulikana kama Z-KILIMO.
Kupitia huduma hiyo ya Z-KILIMO, wakulima vijijini wataweza kupata taarifa sahihi na kwa wakati na hivyo kuendeleza sekta hiyo nyeti kwa maendeleo ya nchi.
"Tunapongeza hatua kama hizi, lakini bado juhudi zaidi zinatakiwa ili kufikia walengwa wengi zaidi” alisema

No comments:

Post a Comment