Na Florah Temba, Same
HALMASHAURI za wilaya mkoani Kilimanjaro zimetakiwa
kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake kutafuta vyanzo vingine vya
mapato, vitakavyowasaidia kupata fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi
mbalimbali ya maendeleo badala ya kukaa kusubiri bajeti za Serikali.
Rai
hiyo ilitolewa jana wilayani Same na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama
wakati akikabidhi vifaa vya kupima ardhi katika halmashauri ya wilaya hiyo
vyenye thamani ya sh. milioni 38 na gari kwa ajili ya ukusanyaji mapato lenye
thamani ya Sh.mil.73.25 ambavyo vimenunuliwa na halmashauri hiyo kwa lengo la
kupima kuongeza mapato ya Halmashauri.
Gama
alisema ni lazima halmashauri za wilaya ziwe na ubunifu na zitafute vyanzo
vingine vya mapato, ili kuondokana na utegemezi wa bajeti ya Serikali ambayo
imekuwa haitoshelezi kufanya shughuli zote za kimaendeleo katika halmashauri.
"Bila
kuwa na ubunifu wa kutafuta vyanzo vya mapato hamuwezi kuendesha halmashauri na
badala yake mtaendelea kulalamika, sasa niwatake muache kufanya kazi kwa mazoea
na mtafute vyanzo vingine vya mapato," alisema Gama.
Aidha Gama aliipongeza
halmashauri hiyo kwa kutafuta njia ya kuongeza mapato katika halmashauri na
kuwataka watendaji kuhakikisha vifaa vilivyonunuliwa vinatumika katika malengo
yaliyokusudiwa.
Alisema wapo baadhi ya
watumishi ambao wamekuwa wakikabidhiwa mali za umma na kuzifanyia ubadhirifu,
hali ambayo Serikali haitaweza kuifumbia macho na badala yake itahakikisha wale
wote watakaobainika kufanya hivyo wanawajibishwa na kuchukuliwa hatua.
Hata hivyo mkuu huyo wa
mkoa alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Joseph Mkude
kuangalia namna ya halmashauri hiyo itaweka utaratibu wa kuingia mkataba na
wale watakaokabidhiwa vifaa ili kuwa rahisi kuwawajibisha pindi
watakapovifanyia hujuma na ubadhirifu.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Same, Mkude alisema uwepo wa vifaa hivyo
kutaiwezesha halmashauri hiyo kupima viwanja ambapo kwa sasa imelenga kupima
viwanja 3, 000 lengo likiwa ni kuweka mji katika hali ya mpangilio.
Aliongeza kuwa
halmashauri hiyo pia imenunua gari aina ya Toyota Hilux Double cabin kwa
gharama ya shilingi milioni 73.25, fedha ambazo zimetokana na mapato ya ndani
ya halmashauri hiyo na vyanzo vingine vya vilivyoko nje ya bajeti ya Serikali
kwa mwaka wa fedha 2012/13.
"Gari hili limelengwa kutumika katika idara ya
fedha kitengo cha mapato, pamoja na kazi zingine ili kuweza kuboresha shighuli
za ukusanyaji wa mapato katika halmashauri yetu, lakini pia ununuzi wa vifaa
vya kupimia ardhi ni hatua kubwa katika kuhakikisha mji unapangwa na wananchi
No comments:
Post a Comment