12 July 2013

CHADEMA KUANIKA VITENDO VYA GREEN GUARD HADHARANI


 Na Rehema Mohamed
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo kinatarajiwa kuonesha kwa v i e l e l e z o kwa waandishi wa habari jinsi Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kutumia kikundi chake cha ulinzi cha Green Guard ambavyo kimekuwa kikipiga watu pamoja na waandishi wa habari kwenye mikutano ya chaguzi mdogo nchini.
Pia chama hicho kimeshangazwa na kauli ya Jeshi la Polisi ya kutishia kukichukulia hatua wakati ikijua wazi kwamba CCM ndiyo mwanzilishi wa vikundi vya ulinzi ndani ya vyama vya siasa.

Akizungumza na gazeti hili Ofisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene, alisema chama hicho kitaonesha kwa vielelezo jinsi Green Guard ambavyo imekuwa ikiumiza watu.
"Kama Polisi wanasema hawajui hilo watueleze maana ya guard nini...CCM wamekuwa wakionesha vijana wao vitendo v y a u k a k ama v u kwe n y e televisheni, lakini chombo hicho kimekuwa kimya," alisema.
Alisema inashangaza kusikia Polisi wanasema ndiyo mara ya kwanza kusikia chama cha siasa kinakuwa na kikundi cha ulinzi. "Kama imekuwepo muda wote iweje polisi wasichukue hatua," alihoji.
Wakati huo huo, chama hicho kinatarajia kufanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Ukombozi, Manzese jijini Dar es Salaam na kueleza msimamo wake kuhusu rasimu ya katiba pamoja na kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na Rais Jakaya Kikwete, wakati akifunga kongamano la amani lililoandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) wakati wa kufunga maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jijini Dar es Sala juzi.

No comments:

Post a Comment