24 July 2013

BARCLAYS YATOA MILIONI 120/- KUSAIDIA VIJANANa David John
BENKI ya Barclays k u s h i r i k i a n a n a taasisi ya Nkwamira imeanzisha mkakati wa kusaidia vijana ambao wamemaliza elimu ya kidato cha nne na sita na kushindwa kufanya vizuri katika mitihani yao na kukaa mitaani bila kujishughulisha.Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Meneja   Mawasiliano wa benki hiyo Tunu Kavishe alisema benki yake imetoa kiasi cha sh. milioni 120 kwa taasisi hiyo kwa lengo la kuwasaidia vijana hao kwa ajili ya kuwapatia mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali.

  Kavishe alisema utaratibu wa k uwa p a t a v i j a n a utafanyika katika mikoa miwili ambayo ni Dar es Salaam pamoja na Morogoro na vijana wanaotakiwa kwa kuanzia ni 100 kati yao 60 watatoka Dar es Salaam na 40 watatoka Morogoro" M p a n g o h u u utawashirikisha vijana 60 kwa Mkoa wa Dar es Salaam na wengine 40 watatoka Morogoro na hiyo itatokana na mitihani mbalimbali ambayo itaendeshwa na wataalamu wa biashara na fedha kutoka vyuo vikuu vya Tanzania," alisema Kavishe.
   Aliongeza kuwa vijana wanaotakiwa ni kuanzia umri wa miaka 15 hadi 35 ambao watachujwa ili kupatikana washindi wawili katika mafunzo na kuendelea nao.Kwa u p a n d e wa k e Mkurugenzi wa Taasisi ya Nkwamira, Noreen Mazalla alisema msaada huo utaweza kuwapatia vijana fursa ya kujiendeleza na kuondokana na hali ya kuwa tegemezi katika familia zao.

No comments:

Post a Comment