24 July 2013

VODACOM YAZINDUA UTOAJI ELIMU



 Na Mwandishi Wetu
WATA N Z A N IA wana kila sababu y a k u f u r a h i kufuatia uzinduzi wa mpango wa mfuko wa kusaidia Jamii yaani Vodacom Foundation uliolenga kutoa nishati ya jua kwa shule zisizo na huduma hiyo nchi nzima. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfuko huo katika Shule ya Sekondari Janguo wilayani Kisarawe, jana Mkuu wa Mawasiliano wa Kampuni mama ya Vodacom, Bi.Suraya Hamdulay, alisema matumaini ya mpango huo uliolenga kutoa nishati ya jua utaendana na mkakati wa kukuza viwango vya elimu nchini.

Alisema kuwa mpango huo ambao utafaidisha mamilioni ya Watanzania hususan waishio maeneo yasiyo na umeme, umekuja wakati ambapo serikali ipo mbioni kufikia malengo iliyojiwekea ya Dira ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya Mwaka 2013 (MDGs) ambayo yanalenga katika kutoa elimu njia rahisi na nafuu kwa wote.
"Mpango huo unahusisha upatikanaji wa nishati ya jua kwenye shule nchini umelenga katika kueneza nishati hiyo katika shule nyingi kwa kadiri inavyowezekana,
Mradi huu umezingatia utunzaji wa mazingira na umelenga katika kuwapatia wanafunzi mazingira mazuri ya kujisomea kitu ambacho kitawapa muda zaidi wa kujifunza na hivyo kuboresha utendaji wao," alisema Bi.Suraya.
Akitoa shukrani zake kwa Vodacom Foundation, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Fatma Kimario, ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi huo, alisema kuwa hatua hiyo ya mpango wa mfuko huo wa kusaidia jamii wa Vodacom F o u n d a t i o n u t a s a i d i a kuboresha upatikanaji wa elimu sambamba na kuboresha utendaji wa wanafunzi nchini.
"Ninaomba wanafunzi kuutumia vyema mpango huo ili kuboresha elimu zao. Ninaamini kwamba kuanzia sasa watakuwa na muda mwingi wa kujisomea yote hii ikiwa ni kutokana na kuwezeshwa kupata nishati ya jua kupitia mradi huu wa Vodacom Foundation. Huu ni mpango mkubwa na ninashukuru Vodacom Foundation kwa kuona umuhimu wake na kuuanzisha," alisema Bi. Kimario.
Mkuu wa Mfuko huo wa Kusaidia Jamii wa Vodacom Foundation, Bw. Yessaya Mwakifulefule, alisema kuwa kiasi cha zaidi ya sh.bilioni 6 kimetengwa kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu nchini kwa mwaka huu

No comments:

Post a Comment