24 July 2013

AUWAWA AKIGOMBEA MSICHANA WA MIAKA 16Kassim Mahege na
Esther Macha
MKULIMA mmoja ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Nkwangu Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya ameuawa kikatili baada ya kupigwa fimbo kichwani kutokana na ugomvi wa kugombea msichana.Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa jana kwa vyombo vya habari na kamanda wa polisi mkoani humo, Kamishna Msaidizi wa Polisi Diwani Athumani, alisema mkulima huyo aliyetambulika kwa jina la Seni Sandu (20) alifikwa na mauti wakati aliposhambuliwa na mkulima mwenzake, Tolo Seko (20) ambao wote ni wakazi wa Kijiji cha Nkwangu.

Alisema kuwa, tukio hilo lilitokea Julai 21, mwaka huu, saa 5 usiku,ambapo Bw.Seko alimshambulia kichwani Bw.Sandu na kumsababishia kifo ambapo chanzo chake ni wivu wa mapenzi; walikuwa wakimgombania msichana (16) jina tunalo.
“Mt u h umiwa b a a d a ya kufanya tukio hili alikimbia lakini kutokana na ushirikiano wa wananchi kijijini hapo walifanikiwa kumkamata na kumfikisha kwenye vyombo husika, tunashukuru ushirikiano wa wananchi waliofanya,” alisema Kamanda Diwani.Kama n d a At h uma n i alisema kuwa mtuhumiwa amekamatwa na taratibu za kumpeleka mahakamani zinaendela ili sheria ichukuwe mkondo wake. Hata hivyo, Kamanda Athuman ametoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria na kudhibiti hasira zao kwa kuyatatua matatizo ya kimapenzi kwa njia ya mazungumzo ili kuepusha ma d h a r a y a n a y owe z a kujitokeza

No comments:

Post a Comment