Na John Gagarini, Kibaha
MAOFISA wa Serikali kwenye idara ya mifugo wametakiwa kutumia
uzalendo wakati wa kuagiza dawa ili kuepuka kuingizwa dawa zisizo na viwango.Hayo yalisemwa mjini Kibaha na
mwakilishi wa kitaifa wa kampuni ya Laprovet ya nchini Ufaransa E p h r a h i m
Ma s s a w e alipoongea na waandishi wa habari na kusema kuwa baadhi ya maofisa
hao wamekuwa wakiagiza dawa zisizo na viwango.
Massawe alisema kuwa kutokana na
kuagizwa dawa zisizo na viwango kumesababisha madhara makubwa kwa mifugo ikiwa
ni pamoja na kufa hivyo wafugaji kupata hasara kubwa."Ku f a kwa mi f u g o kunatokana
na magonjwa mbalimbali hapa nchini kutokana na baadhi ya dawa kuwa kwenye
kiwango cha chini hivyo kushindwa kuzuia au kutibu magonjwa yanayokabili
mifugo," alisema Massawe.
Aidha, alisema kuwa tatizo kubwa ni
ubadhirifu na kutokuwa na uadilifu kwa maofisa hao hali ambayo inasababisha
mifugo mingi kufa kwa kupata matibabu ambayo hayalingani na uwezo dawa hizo
toka nje ya nchi."Maofisa hao baadhi yao si
waaminifu kwani huagiza dawa ambazo hazina viwango licha ya kuwa dawa nzuri
zipo hasa baada ya kuingia soko huria, hivyo wasiangalie maslahi binafsi bali
waangalie utu na uzalendo kwa nchi yao," alisema Massawe.
Massawe ambaye pia ni makamu mwenyekiti
wa Waganga Wasaidizi wa Mifugo nchini (TAVEPA) alisema kuwa, endapo maofisa hao
watakuwa waadilifu watasaidia kuboresha kipato cha wafugaji.Alibainisha kuwa ili kuhakikisha wafugaji wanajua matumizi sahihi
kampuni hiyo inatoa mafunzo pamoja na ushauri wa namna ya ufugaji wa kisasa ili
kuongeza tija kwani ufugaji ni mkombozi wa nchi kwani inaliingizia pato kubwa
la taifa.
No comments:
Post a Comment