Na Mashaka Mhando, Korogwe
MBUNGE wa Jimbo la
Korogwe Vijijini, Stephen N g o n y a n i ' P r o f e s a Majimarefu' kwa siku
tatu mfululizo amekuwa akikesha katika Kijiji cha Magamba Kwalukonge kusimamia
uchimbaji wa kisima ili kutatua kero ya maji inayowakabili wananchi wa kijiji
hicho.
Mwandishi wa habari hizi, alimshuhudia mbunge huyo akishinda na
wananchi wake wakifuatilia uchimbaji wa kisima hicho unaofanywa na Kampuni ya
Sum-Hidrogeo Works ya jijini Dar es
Salaam.
Hata hivyo, eneo ambalo lilipangwa na wataalamu wa maji kuchimbwa
halikuwa lenyewe na hakukuwa na mtu yeyote aliyetajwa kuonesha eneo
lisilopangwa ambalo mkandarasi huyo alipochimba na kufika urefu wa mita 120,
hakukuwa na maji yaliyotoka.
Mbunge huyo baada ya kuona mkandarasi amechimba umbali huo huku
maji yakiwa hayana dalili kupatikana, aliamua kushika chombo kinachopima maji
kisha kuyatafuta katika eneo lingine ambalo aliwahamisha wataalamu hao ambao
walichimba mita 103 wakapata maji.
"Tunamshukuru mbunge wetu tumepata maji katika kijiji chetu,
tulilazimika kulala nje ya nyumba zetu kutafuta maji lakini sasa tunafurahi
kupata maji haya," alisema Mwanaisha Lusewa.
Akizungumza mara baada maji kupatikana mbunge huyo alisema kuwa
ameweza kutatua kero hiyo ya maji katika kijiji hicho baada ya kupata msaada wa
kiasi cha shilingi milioni 20 kutoka kwa kada wa CCM, Mustapha Sabodo kati ya
shilingi milioni 41 alizompa.
Alisema amepata msaada wa kuchimbiwa visima viwili katika kijiji
hicho na kingine cha Kijango kilichopo Kata ya Magoma msaada ambao utamwezesha
kusaidia maendeleo kwa wapiga kura wake.
No comments:
Post a Comment