31 May 2013

Wazazi Masasi wahimizwa kupeleka watoto shule

Na Said Hauni, Lindi


 WA Z A Z I Wi l a y a y a Masasi mkoani Mtwara wamesisitizwa kuwapeleka watoto wao shule ili waweze kupata haki zao za msingi katika kupata elimu itakayoweza kuwasaidia kuendesha maisha yao ya sasa na ya baadaye
Rai hiyo ilitolewa na Kaimu Ofisa Elimu shule za msingi wilayani humo, Said Nanjayo, alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Walemavu wa ugonjwa wa Ukoma katika kijiji cha Mkaseka, Jimbo la Lulindi, wakati wa uzinduzi wa jengo la darasa moja la awali lenye thamani ya sh.milioni 9.
Akizungumza baada ya ufunguzi wa darasa hilo, Nanjoyo alisema ni vema wazazi walio na watoto walio na umri wa kuanza masomo ya awali kuwapeleka mara moja kwenye shule hiyo ili waweze kuanza kupata elimu itakayowawezesha kuingia darasa la kwanza kwenye shule ya
msingi.
Nanjayo alisema ni vema kwa wazazi walio na watoto wenye umri unaostahili kuanza masomo wakafanya hivyo mara moja ili vijana wao walio bado waipate haki yao ya msingi ya elimu ikiwa ni pamoja na kulitunza jengo hilo.
"Kujengwa kwa jengo hili ni si dogo, kwani ni mwanzo wa maendeleo kwenye maeneo yao kwani uwezi kupata maendeleo bila ya kuwa na elimu," alisema Nanjayo.
Pia,aliwasisitiza wananchi wa Kijiji cha Mkaseka kujenga ushirikiano mzuri na shirika la kuondoa unyanyapaa na kuzuia ulemavu utokanao na Ukoma kwa ajili ya maendeleo yao.
Nanjayo aliwataka walimu w a l i o c h u k u a j u k umu l a kuwasomesha vijana hao kufanya kazi zao kwa moyo mmoja ili kuwatia moyo wazazi kwamba watoto wao wanaowafundisha wanapata elimu itakayowasaidia katika maisha yao ya baadaye na Taifa kwa ujumla wake.
Kaimu Ofisa elimu huyo kwa shule za msingi alisema ujenzi wa chumba cha darasa hilo,ni mwanzo wa kuweza kupata shule ya msingi, ikiwemo ya Sekondari katika kijiji chao na kata kwa ujumla wake.
Diwani wa Kata hiyo ya Lulindi, Mussa Mtanga amelishukuru shirika hilo kwa kazi nzuri waliyoifanya ya ujenzi wa chumba hicho cha darasa katika kijiji hicho,kwani kumewapunguzia vijana wao wadogo kutembea mwendo mrefu wa kilomita nne hadi Kijiji cha Ndwika kufuata shule.
Mwanzoni akitoa taarifa fupi,mwakilishi wa Shirika la GLRA l a Uj e r uma n i , t awi l a T a n z a n i a , B u c h a r d Rwamtoga,alisema Jengo hilo lenye chumba kimoja na Ofisi zake mbili, limegharimu sh. milioni 6 kati ya milioni 9 kama ilivyokadiriwa hapo mwanzoni kabla ya ujenzi wake, ambapo kwa upande wa Shirika la (GLRA) likichangia Sh,4.0 milioni ambapo upande wake jamii ikichangia sh.milioni 2.
Alisema ujenzi wa darasa hilo la awali ni sehemu ya uendelezaji wa uhusiano mzuri kati ya wananchi wa Kijiji cha Mkaseka na shirika hilo la Kijerumani lenye tawi lake hapa nchini.
Naye Mtendaji wa kijiji hicho ambaye pia ni mmoja wa walimu wa watoto hao, Juliana Ajetu alisema kituo hicho cha shule ya awali kina wanafunzi wapatao 47 wakiwemo 27 wavulana na wasichana 20.

No comments:

Post a Comment