MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Paschal Mabiti amewataka wanasiasa mkoani humo
kuacha mara moja tabia za kuwadanganya au kuwapotosha wananchi kuhusu kilimo
cha mkataba hususani zao la pamba.
Alisema, yeyote
ambaye ataenda kinyume na agizo hilo atakamatwa ili kufikishwa
mahakamani,
sheria ichukue mkondo wake.
Hayo aliyasema
jana ofisini kwake mjini Bariadi wakati akizungumza na waandishi wa habari
ambapo alikuwa anazungumzia juu ya zao la pamba msimu huu.
Alisema kuwa, katika msimu uliopita
wa zao hilo baadhi ya wanasiasa walipita kwa wakulima kuhamasisha wakatae
kilimo cha mkataba kwa madai wakijiunga watanyang'anywa mashamba yao na wafanyabiashara.
Mkuu huyo alisema, baada ya wakulima
kuambiwa hivyo na wanasiasa hao waliokuwa wame j i u n g a wa l i a n z i s h a
mgogoro mkubwa kati yao na wafanyabiashara hadi kusitishwa kwa kilimo hicho.
Kutokana na hali hiyo, Mabiti aliamua
kupiga marufuku kwa mwanasiasa yeyote atakayebainika anapinga kilimo cha
mkataba kwa msimu ujao kuwa atakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa
ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
Alibainisha kuwa, hali ya zao la
pamba kwa msimu huu ni mbaya katika uzalishaji wake kuwa mdogo, na kutaja
sababu kuwa ni kusitishwa kwa kilimo cha mkataba baada ya kuwepo mgongano baina
ya wahusika katika kilimo hicho.
Pia alisema, kwa sasa serikali
pamoja na wadau wengine wa zao la pamba wakiwemo wafanyabiashara wanafanya
utaratibu wa haraka na ambao utakuwa ni mzuri kuhakikisha kilimo hicho kinarudi
ili kumkomboa mkulima.
“Katika utaratibu utakaowekwa hivi
karibuni, mtu yeyeyote ambaye ni mwanasiasa atakayeonekana na kubainika
anapinga kilimo hicho sitamuonea huruma, nitamkamata na kumchukulia hatua za
kisheria labda aongelee nje ya mkoa wangu,”alisema Mabiti.
Alibainisha kuwa, wanasiasa hao
wamekuwa wakifanya hivyo kwa maslahi yao binafsi na kusababisha wananchi wengi
hasa wakulima kubaki maskini na hata bila kutoa msaada wowote kwa watu hao.
No comments:
Post a Comment