15 May 2013

Mapepo yazua tafrani shuleni



Na Ester Maongezi
Wanafunzi wa kike 32 wanaosoma katika Shule ya Sekondari Manzese, iliyopo Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, jana walianguka wakiwa darasani na kupoteza fahamu.
Tukio hilo ambalo limetokea saa tatu asubuhi, limehusishwa na imani za kishirikina ambapo uongozi wa shule ulilazimika kuwaruhusu wanafunzi wengine
kurudi majumbani kwao.
Akizungumza na gazeti hili, Mkuu wa shule hiyo, Bw. Linus Mwakasege, alisema tukio hilo limekuwa likijirudia mara kwa mara kwa siku za Jumatano na Ijumaa.
“Idadi ya wanafunzi waliokuwa wa k i a n g u k a k a t i k a s i k u hizi ni ndogo ambayo huwezi kuilinganisha na tukio la leo (jana) ambalo limetushtua sana,” alisema Bw. Mwakasege.
Akielezea mazingira ya tukio hilo, Bw. Mwakasege alisema alianza mwanafunzi mmoja kupiga kelele akiwa darasani, kuanguka chini na kupoteza fahamu.
Alisema hali hiyo iliendelea kwa wanafunzi wengine hadi ilipofikia idadi hiyo na wengine kukimbia ovyo ambapo walimu walifanya kazi kubwa ya kuwatuliza.
Bw. Mwakasege alisema baada ya tukio hilo, alifanya jitihada za kuita viongozi wa dini ya Kikristo na Kiislamu ambao walifika shuleni hapo na kuwaombea wanafunzi waliopatwa na tatizo ambapo hali hiyo iliwasaidia kurudi katika hali ya kawaida.
Mwanafunzi mmoja wa shule hiyo ambaye naye alipatwa na tatizo hilo, Hellen Said alisema hakuwa akifahamu lolote bali alijikuta mapigo ya moyo yakimuenda mbio, kuanguka na kupoteza fahamu.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Manzese, Bw. Salehe Rashidi, alisema tukio hilo limekuwa likijirudia shuleni hapo hivyo atashirikiana na uongozi wa shule kuhakikisha kila mwanafunzi kwa imani yake wanafanya maombi kila wiki.
“Maombi haya yatasaidia kukabiliana na mapepo mabaya yanayowaandama wanafunzi ambao wanakosa uhuru wa kusoma ili kujiwekea msingi mzuri.wa ,aisha alisema.

No comments:

Post a Comment