*NI KUTOKANA NA KAULI YAKE KUHUSU URAIS 2015
*MANGULA ASEMA NEC HAIJATANGAZA MCHAKATO KUANZA
*ASISITIZA WATAKAOJITANGAZA WATAKATWA
WAKATI Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta
akijipambanua wazi kuwa yeye na mawaziri wenzake watatu wanaoendana kimawazo
watakaa na kuangalia mmoja wao awanie urais mwaka 2015 , Makamu Mwenyekiti wa
CCM (Bara), Philip Mangula, amesema wanaofanya hivyo wanakiuka katiba ya CCM
hivyo wakati ukifika watakatwa majina yao.
Mangula alitoa
kauli hiyo juzi wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari mara baada ya
kuzindua kampeni za mgombea udiwani wa CCM katika Kata ya Iyela, jijini Mbeya.
Alisema Katiba
ya chama hicho iko wazi na inataka wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi
kupitia CCM kusubiri wakati nafasi husika zitakapotangazwa.
Alisema kufanya
hivyo kabla ya kutangazwa ni kutomtendea haki kiongozi
aliyeko madarakani
ambaye ndiye anayetekeleza ilani ya chama.
Mangula
alisisitiza kuwa n i ma k o s a ma k u bwa kwa mwanachama yeyote kuzunguka
wakati huu na kujitangaza kuwa atawania urais mwaka 2015, kutokana na ukweli
kuwa tayari nchi inaongozwa na Rais anayetoka CCM ambaye ni Rais Jakaya
Kikwete.
“Hivyo kutangaza nia kabla ya wakati
ni makosa makubwa,” alisisitiza. Alisema kuwa kama chama hicho kitakuwa na
ushahidi wa kutosha kuwa kuna wanachama walijitangaza mapema kabla ya wakati
kutangazwa ni wazi kuwa vikao vya mchujo vitawachuja na kuwaondoa katika orodha
ya wanaowania nafasi hiyo na kubaki na wagombea waliofuata kanuni na katiba ya
chama hicho.
Alisema watakaobainika tutawakata
majina yao kwa kuwa ni NEC tu yenye mamlaka ya kutangaza wakati wa kujitangaza.
Kwa upande wa nafasi za ubunge na
udiwani katika maeneo ambayo yanaongozwa na upinzani mwanachama wa CCM,
anaruhusiwa kupitapita kwa ajili ya kuangalia hali ya hewa na kuwafanya
wanachama kumfahamu ili wakati ukifika aweze kujitosa rasmi katika
kinyang’anyiro ili kukomboa nafasi hiyo.
Hivi
karibuni waziri Sitta akiwa anaongoza harambee katika Kanisa Katoliki la Mt.
Josephine alidaiwa kutamka wazi kuwa yeye na rafiki zake Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Ujenzi, Dkt.John Magufuli
na Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, kwa kuwa ndio anaoendana nao
kimawazo na kimsimamo wa kutopenda kuwaonea wanyonge, watakaa na kuona mmoja
wao agombee urais.
YAO
Hao ni chui waliovaa ngozi ya kondoo katika chama chetu hatutaki wanafiki na wasaliti wa chama kwa kujitafutia umaarufu usio na tija na sisi Watanzania hatuwezi kamwe kumchagua raisi mnafiki kama kafanya hivyo leo itakuwaje wakiwa maraisi si watatusaliti watanzania.
ReplyDelete