30 May 2013

‘Mgonjwa wa akili’ aua watoto, ajeruhi


Livinus Feruzi, Bukoba
na Thomas Kiani, Singida


 MTU anayedhaniwa kuwa na matatizo ya akili amewaua watoto wawili kwa kuwakatakata mapanga na kumjeruhi mama yake mzazi pamoja na mtoto mwingine wa darasa la saba, wote wakiwa ni wa familia moja.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Bw. Philip Kalangi, alisema tukio hilo lilitokea Kata ya Kamachumu wilayani Muleba. Kamanda Kalangi alimtaja mtuhumiwa wa mauaji hayo kuwa ni Salvatory Sylivester (30), mkazi wa Kikomero.
Waliouawa katika tukio hilo kwa mujibu wa Kamanda Kalangi ni Kevin Antidius (3) na Julieth Julius (5). Waliojeruhiwa ni mama yake mzazi, Valentine Sylvester (69) na Kabyemera Sylvester (7), ambaye anasoma darasa la kwanza.
Kamanda Kalangi alisema mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi. Alisema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa mtuhumiwa alikuwa na matatizo ya akili. Alisema polisi wanaendelea na
uchunguzi na kuwa mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
Katika tukio la pili, mwanafunzi wa kidato cha pili Shule ya Sekondari ya Kagemu, Umud Buruan (17) amefariki baada ya kuchomwa jichoni na mwamvuli na mwenzake.
Akielezea tukio hilo, Bw. Kalangi alisema jana saa 10:30 wakati wanafunzi wakitoka shuleni kwenda nyumbani walianza kutaniani, ambapo, Machel Omugisha (16) alikasirika na kumchoma mwezake sehemu ya jicho kwa kutumia mwamvuli aliokuwa nao.
Mwanafunzi huyo alifariki baada ya kufikishwa katika hospitali ya Mkoa wa Kagera wakati akipatiwa matibabu na kuwa tayari mtuhumiwa anashikiliwa na polisi.
Wakatu huo huo, Jeshi la Polisi mkoani Singida limemtia mbaroni mkazi mmoja wa Kijiji cha Musimi Kata ya Sepuka Wilayani Ikungi, Swalehe Mohamed (42) maarufu kwa jina la ‘Kipara’ kwa tuhuma za kumuua mama yake wa kufikia kwa kumkata kata kwa panga mikono yote miwili na kwenye makwapa yote mawili.
Katika taarifa yake kwa waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi mkoani Singida, Jofrey Kamwela, alisema tukio hilo lilitokea jana

No comments:

Post a Comment