SAKATA la kupinga ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es
Salaam, bado ni tete baada ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)
kubaini kuwepo kwa vijana wanaoapishwa viapo na wazee wa kimila kuhakikisha
gesi hiyo haitoki.
Akizungumza na waandishi wa habari
Jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Harold Sungusia,
alisema utafiti wao umebaini jinsi kiapo hicho kinavyofanyika.
Alisema wananchi hao w amemw a g a d
amu y a mbuzi wawili ili kukamilisha matambiko na imani za viapo hivyo kimila.
“Kutokana na utafiti, tumeona
umuhimu wa kutoa tamko kwenu ili mtusaidie kueleza jamii, Serikali na wananchi
wa Mtwara kuwa kuendelea kuamini kuwa hali ya Mtwara ni shwari sawa na kufunika
moto kwa blanketi, kwani vijana wetu wanaendelea kula viapo vya kuhakikisha
gesi haitiki,”alisema
Aliongeza kuwa katika utafiti huo
wameweza kuongea na wazee hao
wa kimila na kuwahakikishia kuwa kati ya mbuzi
hao, ambao mmoja alichinjwa eneo la Msimbati ambapo kutajengwa bomba la gesi,
ikiwa ni ishara ya kuhakikisha gesi, haitoki ,” alisema.
Alisema mgogoro huo ambao umeleta
madhara kutokana na vurugu za Mei 22, mwaka huu umesababisha vifo na mauaji,
uharibifu wa mali, kukosekana kwa amani kati ya wananchi na vyombo vya usalama.
Sungusia aliitaka Serikali kuboresha
vyombo vyake vya usalama na kufanya mabadiliko ili kurejesha uhusiano mzuri na
wananchi.
Pia wameshauri kamati teule
iliyoundwa na Bunge kufika Mtwara na kufanya mazungumzo na wananchi ili kupata
taarifa sahihi na kutafuta mbinu mbadala za kurejesha amani ya kudumu.
K w a u p a n d e w a k e
Mwanasheria wa LHRC, Bi Grace Mwangamila, alisema kutokana na tafiti hiyo
wamegundua kuwa wananchi wa Mtwara bado wana roho ya kinyongo.
CUF
yaandaa kongamano
Kwa upande wake Chama cha Wananchi
(CUF), kinaandaa kongamano maalum kwa ajili ya wananchi wa Mkoa wa Mtwara na
Lindi wanaoishi jijini Dar es Salaam, ili kuwaelimisha kuhusiana na hasara na
faida zinazotokana na gesi.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro, alisema
mkutano huo utafanyika Juni 2, mwaka huu katika ofisi za chama hicho kutokana
na maombi ya wananchi hao.
Alisema wameamua kufanya mkutano huo
jijini Dar es Salaam baada ya Serikali kupiga marufuku mikutano ya wanasiasa na
asasi za kiraia mkoani.
“Tumeamua kufanya mkutano huu kwa
ajili ya kuwaelimisha Watanzania wenzetu ambao hawajui hadi sasa gesi ina faida
gani na hasara zipi, hivyo tutawaeleza suala zima la uwekezaji katika sekta
hii,”alisema Itatiro.
A l i o n g e z a k w a m b a
inawezekana fujo zao zinatokana na kutoelewa lolote juu ya suala la gesi . Pia
alisema katika kongamano hilo wananchi wataandika maoni mbalimbali ambayo
yatakusanywa na kupelekwa katika Ofisi ya Rais, Ofisi ya Wazuri Mkuu, na Spika
wa Bunge.
CEGODETA
Nayo Taasisi ya Utawala Bora na
Maendeleo Tanzania (CEGODETA) imeitaka Serikali kuhakikisha inafanya uchunguzi
wa kina na kuwachukulia hatua wanasiasa wote watakaobainika kuhusika na vurugu
za Mtwara na kusababisha watu kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa bila kujali
nyadhifa zao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa
kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na kusainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa
CEGODETA, Thomas Ngawaiya, ililaani vikali vurugu hizo na kuitaka serikali
kuwachukulia hatua wahusika wote.
N g a w a i y a a l i s e m a
kutokufanya hivyo kutaifanya Tanzania kuonekana ni nchi isiyotawalika kama
baadhi ya nchi za Kiafrika zilivyo.
“CEGODETA inaamini kwamba vurugu za
Mtwara zina mkono wa kisiasa, hivyo serikali ifanye uchunguzi wa kina na
kuwachukulia hatua wanasiasa wote watakaobainika kuhusika na vurugu hizo bila
kujali ni vyama gani au wana wadhifa gani ndani ya vyama vyao, vinginevyo
Tanzania itakuwa ni nchi isiyotawalika,” alisema.
Alionya wanasiasa wanaotaka kutumia
vurugu ili kuingia madarakani kuacha mara moja kwani wanapaswa kuelewa kuwa
amani ya nchi itakapovurugika hata wao watadhurika.
Aliitaka Serikali ichukue hatua
zinazofaa kuhakikisha matukio kama hayo hayajirudii tena mkoani Mtwara na nchi
nzima.
Ime a n d i k w a Ma r i a m Mziwanda, Rehema Maigla na Rose Itono
No comments:
Post a Comment