24 May 2013

Sheha amwagiwa tindikali Zanzibar


Mwajuma Juma na Mariam
Mziwanda


 SHEHA waShehia yaTomondo, Zanzibar, Bw.Mohammed Saidi Kidevu ,amemwagiwa tindikali akiwa nyumbani kwake Tomondo, Wilaya ya Magharibi Unguja.
Tukio hilo limetokea saa 2:30, usikuwa kuamkia janawakati akichotamaji.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Hospitali yaMnazi mmoja,Bw.Kidevu w akatiakiendelea kuchotamaji, alitokea kijana mm oja as iyemfahamu nabaada yakusalim alim mwagia tind ikali.
Alisema baadaya kumwagiwatindikali,alijaribu kumkimbiza lakini alishindwa kumkamata nahakuwezakupatamsaadawowote kutoka kwa wananchi.
“Awali nilikuwanikipokea vitishokutokakwawatumbalim bali ambao siwafa ham u...v itishohivivilianz aw akati wa chaguzi zaWilayail ikuwapataW ajumbewa Mabaraza ya Katiba,” alisema
Bw. Kidevu.
Kwa upa ndewak e, dakta ri anayemtibuSaidi Ali,amesema
Bw.Kidevu am epatam ajerahakatika jicholakulia ,kifuani namgong onilakini hali yake ina endeleavizu ri.
Aliong ezakuwa, up ouwezekanomkubwawa kuponak wani jicho hilol inaona nahalikua thirikandan ilakinit una sikilizauamuzi waSerikalikama w ataamuakum safirisha katikaHospitali yaMuhimbili, Dar es Salaam,” alis ema.
MakamuwaPiliwaRaisZanzibar, B aloz i Seif Ali Iddi, alifika hospitalini hapo na kulitaka Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina na kuhakikisha mhusika wa tukio hilo anakamatwa.
Alisema Serikali imesikitishwa na kitendo hicho ambacho kinaashiria uvunjifu wa amani na kudai kuwa, Serikali itagharamia matibabu yake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Ali Mkadam, alisema wamekamata chupa yenye maji ambayo yanasadikiwa kuwa na tindikali.
“Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kina...chupa iliyokamatwa itafanyiwa vipimo ili kupata alama za vidole ili kumbaini mhusika...upo uvumi ambao umelihusisha tukio hili na vurugu za kidini na kisiasa hivyo tumejipanga kwa kuweka ulinzi,” alisema.
Desemba 2012, Shekhe Fadhil Soraga ambaye ni Katibu wa Mufti Zanzibar, naye alimwagiwa tindikali katika maeneo ya Mwanakwerekwe

No comments:

Post a Comment